JEE KUISHA KWA MWEZI WA RAMADHANI NDIO MWISHO WA MAMBO MEMA?
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni Mwezi wa Toba, Mwezi wa Ibada ya Funga na Visimamo vya Sunna kama Tarawehe ,Dhikri N.k.
Ramadhani Hiyo inaelekea kuisha.
Jee Kuisha kwa Mwezi wa Ramadhani Ndio Mwisho wa Ibada na Mambo Mema?
JIBU
HAPANA MAMBO MEMA NA IBADA INATUBIDI/TUPASA TUENDELEE NAYO MILELE KWANI WAAJIBU WETU WANAADAMU NA NDIO LENGO KUU LA KUUMBWA KWETU WANAADAMU DUNIANI.
ALIYEKUWA AKIIMUABUDU M/MUNGU KWA AJILI YA MWEZI WA RAMADHANI BASI JUA KWAMBA MWEZI WA RAMADHANI UMEKWISHA NA ALIYEKUWA AKIMUABUDU M/MUNGU KWA DHATI/UKWELI WA KUMUABUDU HUYU ANAJUA KUWA M/MUNGU DAIMA YUPO KATIKA KILA MIEZI NA KILA SIKU NA SI MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI TU.
Lengo kuu la Funga ni kuupata na kuufikia Ucha Mungu .
Ikiwa Umeweza kujizuia na kula na kunywa na mengineyo Ndani ya Mwezi huu .
Tuna Imani kwamba tunaweza kujizuia na Mengine katika Mabaya baki ya Miezi Mengine na hilo ndio lengo kuu.
IANDAE SIKUKUU YA EID .
Indae Sikukuu ya Eid kwa furaha zote Mshukuru M/Mungu kwa kukupa Uwezo wa Kufunga na ukaweza Funga kwani wengi katika sisi walitamani kuwa nasi katika funga ya Mwaka huu lakini kwa Uwezo wake M/Mungu hawakuweza kuitekeleza Ibada hiyo.
Hivyo basi Tumshukuru Sana M/Mungu .
Vaa vizuri , Kula Vizuri , Wanunulie watoto wako zawadi , kuwa karibu na Familia yako , Wasaidie wasio na Uwezo , TOA ZAKKATUL FITRI KABLA YA SWALA YA EID na mengi katika Ratiba za kheri Ulizo zipanga.
Tusirudi Nyuma katika Kufanya Mema na Mazuri Siri ya Mwisho wetu hapa Duniani Mola Ndiye ajue huenda hii ikawa Ndio Funga yetu ya Mwisho ikiwa ndio hivyo.
M/Mungu Tunamuomba atupokee waja wake tukiwa wasafi na wenye kufutiwa Dhambi zetu na kukubaliwa Maombi yetu.
NDUGU ZANGU WAPENDWA TUSIRUDI NYUMA KIIBADA TUSONGE MBELE NA TUZIDISHE IBADA NA MEMA ILI TUPATE RADHI ZAKE M/MUNGU DUNIANI NA KESHO AKHERA TUSIZIAME NYUMBA ZA IBADA TUSIACHE KUWASAIDIA WASIO JIWEZA TUSIZIACHE TABIA NJEMA TULIZO KUWA NAZO KATIKA MWEZI HUU IKAWA TUMERUDI KATIKA MAKOSA AMBAYO HUENDA TUSIDIRIKI TOBA YAKE TENA.
Miongoni Mwa Masharti ya Toba ya Kweli ambayo wanazuoni wametuongoza ni kutorejea katika Makosa ambayo tuliyo yatenda.
Tujipange na kuhakikisha haturudi nyuma katika Mambo ya kheri ili kupata Radhi za Allah Subhanahu wataalllah.
Nimalize kwa Dua Mola tunakuomba Tusamehe Waja wako , yapokee Maombi yetu , Tupe Upendo na Amani katika Nchi yetu ya Tanzania , Usitu adhibu kwa makosa ya Wachache wetu , Wasamehe wazazi wetu walio tangulia Mbele ya haki na Ndugu zetu wote kwa Ujumla,tujaalie kuwa Miongoni wa Wajaa wako walio Udiriki Usiku wa Cheo LAYLATUL QADIR.
Rehma na Amani zimshukie Bwana wetu Mtume Muhammad (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie juu yake na Amani.
NAWATAKIA EID MUBARAKA M/MUNGU AREJESHE FURAHA KWETU SOTE MILELE
Na : Ghalib Nassor Monero L Azhariy
Kijitonyama Ali Mauwa
Dar es salaam , Tanzania

WABILAHI TAUFIQH
NAWATAKIA EID MUBARAKA M/MUNGU AREJESHE FURAHA KWETU SOTE MILELE
Na : Ghalib Nassor Monero L Azhariy
Kijitonyama Ali Mauwa
Dar es salaam , Tanzania
amin insha allah
ReplyDelete