Wednesday, September 25, 2013

ABDULRAHMAN KINANA AWAWEKA SAWA WANA MUSOMA, AWAAMBIA WAHOJI MAENDELEO YAO

2
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amepanda kwenye kivuko cha MV Musoma kinachovusha watu kutoka Wilaya ya Rorya na Musoma kikitokea Kinesi leo akielekea Musoma mjini tayari kwa kumalizia ziara yake mkoani Mara, ambapo amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM, Kinana amemaliza ziara yake ya mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara leo kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara kwenye uwanja wa Mukendo mjini Musoma akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa CCM Nape N nauye.Ndugu Kinana amesema ni haki ya wananchi kuhoji maendeleo yao kwani wanasiasa wa vyama mbalimbali vikiwemo vya upinzani vilipita na kutoa ahadi tena wengine waliahidi kutoa asali na maziwa huku wengine wakiahidi wananchi kuwa wakiwachagua watajenga barabara za marumaru.
3 4 5
Msafara wa magari ukitoka kwenye kivuko cha MV Musoma mara baada ya kuwasili mjini Musoma leo ukitokea wilayani Rorya.
6 7 8 9 10 11 12
Ukaguzi ukiendelea
13 14 15
Hii ndiyo ofisi yenyewe.
16
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akipokea zawadi jogoo kutoka kwamwenyekiti wa shina namba 6 mama ThabithaAmina Idd mara baada ya kutembelea shina hilo na kuongea na wanachama.
17
Katibu Mkuu wa Umoja wa wanawake UWT Mama Amina Makilagi akiwahutubia wana Musoma leo kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mukendo mjini Musoma leo.
18 19
Hawa ni miongozi mwa wananchi waliohudhuria katika mkutano huo leo.
20
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wana Musoma leo.

PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MUSOMA MARA

No comments:

Post a Comment