Sheikh Muhammad Bakar Al burhan, Mudir wa Madrasatil
Shamsul maarif ya Tanga.
Ajali hiyo ilimsababishia majeraha Sheikh Muhammad bakari katika maeneo ya kichwani,kifuani na mikononi.
Na vilevile wengine kupata Majeraha ambao walikuwa katika Msafara huo ambao walikuwemo Mwalimu Mussa Kunema,Idd issa Nori na kambi salum.
Msafara huo Sheikh aliongozana na watoto wake Abdulhalim,Ahmad, Abuubakar pamoja na mkewe.
Msafara huo ulikuwa unatokea Tanga kwenda kondoa kwa ajili ya kutangaza dini.
Majeruhi wote walikimbizwa katika hospitali kuu ya Morogoro na baada ya hapo wali hamishwa kupelekwa hospital kuu ya Muhimbili.
Katika Ajali hiyo Mtoto wa Sheikh aitwaye Abuubakar alifariki pamoja na mke mdogo wa sheikh bi ziyada naye amefariki.
Tunamwomba mwenyezi mungu amfanyie wepesi na kupona kwa haraka sheikh wetu na majeruhi wengine.
Vile vile Mwenyezi mungu awapokee mapokezi mema na awasamehe makosa yao Marehemu zetu wote pia awaingize katika Pepo yake ya Darja ya Juu kabisa.
Amiin
SHEIKH MUHAMMAD BAKAR ATOKA HOSPITALI.
Sheikh alikuwa amelazwa hospitalini hapo tangu siku ya jumanne ya Tarehe 27 akitokea katika hospitali ya mkoa wa morogoro kufuatia ajali ya gari aliyoipata wilaya ya dumila mkoani morogoro.
Aidha kwa sasa Sheikh ametakiwa na madaktari wa MOI waliokuwa wakimtibia kupata muda zaidi wa kupumzika ili kuimarisha zaidi afya yake.
Majeruhi wengine waliopewa ruhusa ni Mwalimu Mussa kunema na Kambi Salumu.
Majeruhi Idd Issa Nori bado yupo hospitali ya Muhimbili wodi ya sewahaji akiendelea kupata matibabu zaidi.
Wakati huo huo imetolewa meseji ya mwisho ya marehemu Abubakar mtoto wa sheikh Muhammad Bakar,aliyoituma siku moja kabla hajafariki katika ajali hiyo ya Dumila.Meseji hiyo aliituma muda wa saa nane za mchana,sawa na muda aliofariki siku iliyofuata.
Baadhi ya watu aliowatumia meseji hiyo ni ustaadh Walid Alhad,imam wa msikiti wa kichangani pamoja na wanafunzi wenzake aliokuwa anasoma nao kwa Sheikh Alhad omar,Magomeni dar es salaam katika madrasatul Tadhwamun.
Meseji hiyo ambayo kama ilikuwa ikibashiri kifo chake na yenye ujumbe mzito wenye kuhitaji kuzingatiwa ilisomeka hivi;
"A,aleykum Pendelea saana kuhudhuria ktk mazishi na usisimame mbali na kaburi kuwa jirani nalo ili uione thamani yetu inavyokuwa baada ya kufa maana ile nguo tunayovishwa huwezi kuivaa ktk uhai na tunaviringishwa kwenye mkeka si tena kitanda kizuri ulichokuwa unalalia kisha tunaingizwa kwenye kishimo kirefu (MWANANDANI) na tunafukiwa udongo juu,hivi thamani yetu iko wapi? mpaka tunashindwa kumuabudu aliyetuumba tatizo nini,muda hatuna? au tatizo ujana?
Kama ujana, vijana wangapi wanaotangulia mbele ya haki kabla ya wazee? kama ni mzee unangoja nini wakati uzee ni dalili ya ukomo wa umri wako? Ni vema tukajiandaa mapema kwa sababu safari ni lazima insha allah mchana mwema".
GARI ALIYOPATA NAYO AJALI SHEIKH MUHAMMAD BAKAR AL BURHAN
No comments:
Post a Comment