Friday, September 27, 2013

INTERPOL WATOA KIBALI CHA KUKAMATWA 'MJANE MWEUPE', ATANGAZWA NDIO MWANAMKE HATARI DUNIANI, NCHI 190 ZILIOMBA KIBALI

Polisi wa Kimataifa,Interpol imetoa kibali cha kutiwa nguvuni mwanamke Mwingereza anayedhaniwa kuwa alihusika na shambulizi lililofanyika dhidi ya jumba lenye maduka la Westgate jijini Nairobi nchini Kenya.

Interpol imesema kuwa kibali cha kutiwa nguvuni Samantha Lewthwaite kimetolewa kwa ombi la serikali ya Kenya kwa tuhuma za kumiliki mabomu na kufanya njama za kutenda uhalifu Disemba mwaka 2011.

Mkurugenzi Mkuu wa Interpol Ronald K. Noble amesema ombi la kutiwa nguvuni mtuhumiwa huyo limewasilishwa kwa nchi 190 wanachama wa Polisi wa Kimataifa.

Awali mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa katika ngazi ya taifa kwa tuhuma za kumiliki pasi bandia ya kusafiria ya Afrika Kusini.

Mwanamke huyo maarufu kwa jina la "Mjane Mweupe" alikuwa mke wa Jermaine Lindsay ambaye alikuwa miongoni mwa waliolipua mabomu katika shambulizi la tarehe 7 mwezi wa 7 mwaka 2005 katika metro ya London ambalo lilisababisha vifo vya watu wasiopungua 52 na kujeruhi mamia ya wengine.  

Website ya Interpol
Samantha Lewthwaite mwenye umri wa miaka 29 anadhaniwa kuwa mwanachama wa kundi la Al Shabab ambalo tarehe 22 mwezi huu lilishambulia jumba la maduka la Westgate jijini Nairobi na kuua watu karibu 70. Samantha ametajwa kwa sasa ndio mwanamke hatari zaidi duniani na anayetafutwa kwa udi na uvumba aidha awe mzima au maiti.
  
 
pasipoti inayomuonesha kama raia wa Afika Kusini 

No comments:

Post a Comment