Saturday, September 14, 2013

KANALI ABDULRAHMAN KINANA AHITIMISHA ZIARA YAKE MKOANI SHINYANGA JANA , LEO KUANZA MKOA MPYA WA SIMIYU

1Mwekezaji wa viwanda wa vya nguo  vya kusindika Pamba na kusokota nyuzi vya Danong Textile Bi. Jing Lin akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wa nne  kutoka  kulia kabla ya kukagua ujenzi wa viwanda hivyo katika ziara yake ya kuimarisha chama na kuhimiza utekelezaji wa  ilani ya Uchaguzi ya chama hicho, Kinana amehitimisha ziara yake leo mjini Shinyanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja  vya Shycom mjini humo.4Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakiingia katika eneo la viwanda vya Danong Textile wakati alipokagua ujenzi wa viwanda hivyo Jana.5Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lu  Yuoqing akimuelezea jambo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akikagua ujenzi wa viwanda hivyo leo, kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi.6Haya ni Maboksi yaliyohifadhi mashine mbalimbali zitakazofungwa katika viwanda hivyo mjini Shinyanga.7Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka katika moja ya mashine za kunyanyulia mizigo katika kiwanda hicho kushoto ni Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lu Youqing.9Baadhi ya wenyeviti wa mashina na matawi katika manispaa ya Shinyanga.10Baadhi ya wenyeviti wa mashina na matawi katika manispaa ya Shinyanga waliohudhuria katika kutano huo.11Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipungia mikono wenyeviti wa matawi na mashina wakati alipowasili kwenye wanja wa Kambarage ambako mkutano wa ndani umefanyika Jana.13Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Lu Youqing akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shycom mjini Shinyanga leo kulia ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi na kushoto Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana.

17Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.19Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Steven Masele akikabidhi matofali elfu kumi na mifuko mia moja ya Saruji kwa ajili ya ujenzi wa zahanati katika moja ya kata za manispaa ya Shinyanga.20Timu ya Stend FC ambao ni mabingwa wa ligi ya Daraja la Kwanza wakikabidhi vikombe vyao kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana Jana21Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akitangaza neema ya umeme vijijini kwa wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Shycom mjini Shinyanga.22Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Steven Masele  na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Ndugu Khamis Mngeja  wakiwasha Pikipiki kama ishara ya kuzizindua kwa ajili ya kukabidhi kwa  watendaji wa chama cha mapinduzi katika ofisi za Chama za Kata mbalimbali, Pikipiki hizo zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Steven Masele mbele ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana.23Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiendesha Baiskeli wakati alipokuwa akiondoka kwenye viwanja vya Shycom mjini Shinyanga mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara Jana jioni.24Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiendesha Baiskeli wakati alipokuwa akiondoka kwenye viwanja vya Shycom mjini Shinyanga mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara Jana jioni.25
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akiwahutubia wananchi waliojitokeza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shycom mjini Shinyanga Jana.


 (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-SHINYANGA)

No comments:

Post a Comment