Monday, September 02, 2013

MKUTANO WA HADHARA UMOJA WA VIJANA WA CCM NA WANANCHI ZANZIBAR

Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Sixtus Mapunda akiwahutubia wakazi wa Zanzibar kwenye viwanja vya Komba Wapya leo tarehe 1 Septemba 2013 mjini Zanzibara mara baada ya kuidhinishwa na wajumbe wa UVCCM mjini Zanzibar kuwa katibu mkuu wa umoja huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (Zanzibar) Ndugu Shaka Hamdu Shaka akihutubia wananchi wa Zanzibar na kuwaahidi kuwa sasa wajiandae kwa mikutano ya mara kwa mara yenye tija ya kuimarisha chama na kudumisha Muungano.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa Sadifa Juma Khamis akihutubia wakazi wa Zanzibar kwenye viwanja vya Komba Wapya.
Sehemu ya wakazi wa Zanzibar wakionekana kuvutiwa na hotuba za viongozi wa umoja wa Vijana.
Wapenzi wa CCM Zanzibar wakiwa wamekaa mpaka juu ya nyumba kusikiliza hotuba za viongozi wao kutoka umoja wa jumuiya ya vijana wa CCM.

No comments:

Post a Comment