Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wazee wa kata ya Isenya wilaya ya Serengeti waliokuja kumpokea.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mwalimu wa masomo ya sayansi Ndugu Silvester Joseph , Katibu Mkuu alitembelea shule ya Natta Secondary na kushuhudia jinsi masomo ya sayansi yanavyopewa kipaumbele.
Mwanafunzi wa Kidato cha Nne Peter Semion wa shule ya sekondari ya Natta iliyopo kata ya Natta wilaya ya Serengeti akimuelekeza namna ya kutengeneza sabuni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipotembelea shule hiyo ya Natta iliyopo wilaya ya Serengeti.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana wajasiriliamali wa kuendesha boda boda na ukulima wa mboga mboga mara baada ya kuzindua kikundi hicho ambapo aliwasihi lazima wapate elimu ya biashara wajue namna ya kuweka na kukopa na kulipa madeni kwa wakati.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka ndani ya ukumbi wa mkutano wa MUGUMU CCM ambapo alikutana na vijana wajasiriamali wa wilaya hiyo.


No comments:
Post a Comment