Sunday, September 15, 2013

MAMA KIKWETE AWATAKA WANAFUNZI WA KIKE KUJIEPUSHA NA MAFATAKI, WANAFUNZI WA KIUME KUTOKUVAA MILEGEZO NA KUVUTA SIGARA

Picha no 1a
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni  mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Kisarawe hivi karibuni wakati alipowasili katika Shule ya Sekondari Msimbu iliyopo wilaya hiyo  mkoani Pwani ili kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi.Fatuma Kimario .
Picha no 2
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi.Fatuma Kimario akisisitiza jambo wakati Mke wa Rais Mama Salma Kikwete  alipotembelea Shule ya Sekondari Msimbu na kuzungumza na wanafunzi wa shule hiyo ambapo aliwaasa wapende shule na kuepukana na mambo mabaya kama vile mafataki na uvutaji bangi ili waweze kufikia malengo waliojiwekea,kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni  mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) anayefuatia ni  Mwenyekiti wa Halmashauri Adam Ng’imba na kulia ni Mwenyekiti wa CCM  Kisarawe Bi.Tatu Kano.
Picha 4
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni  mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Msimbu  iliyopo wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani wakati alipowatembelea hivi karibuni. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya kisarawe Fatuma Kimario,na kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri Adam Ng’imba anayefuatiwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Zipporah Simwanza.
Picha no 7 Picha no 5
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Msimbu  wakisoma shairi la kumkaribisha Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni  Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA) hivi karibuni wakati alipoitembelea shule hiyo iliyopo wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.
 (Picha na Lorietha Laurence-Maelezo)

No comments:

Post a Comment