Makamu
Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua
semina ya mafunzo ya siku nne kwa Watendaji na viongozi wa CCM ngazi za
mikoa na wilaya nchini, katika jengo la White House, Makao Makuu ya CCM
mjini Dodoma leo, Oktoba 21, 2013. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa
CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana,
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM (zanzibar) Vuai Ali Vuai.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa maelezo kuhusu lengo la mafunzo hayo.
Katibu
wa NEC, Itikasi na Uenezi Nape Nnauye akitoa neno la utangulizi kabla
ya kumkaribisha Kartibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuzungumza
kwenye semina hiyo.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM
(Zanzibar), Dk. Ali Mohamed Shein alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa
Dodoma, leo kwa ajili ya kufungua semina hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein mara
baada ya kuwasili katika ukumbini kwa ajili ya kufungua semina ya
mafunzo kwa watendaji na viongozi wa CCM ngazi za mikoa na wilaya, leo
kwenye Jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kulia ni
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba, na Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam
Kimbisa.
Wajumbe wakishangilia, Dk. Shein alipowasili ukumbini. Washiriki wa semina hiyo wakiwa ukumbini.
Wajumbe wakishangilia, Dk. Shein alipowasili ukumbini. Washiriki wa semina hiyo wakiwa ukumbini.
Wajumbe wakishangilia baada ya semina yao kufunguliwa na Dk. Shein.
Makatibu
wa NEC, Zakiah Meghji (Uchumi na Fedha) na Mohammed Seif Khatib
(Oganaizesheni) wakifuatilia kwa makini hali ya mabo ukumbini wakati wa
semina hiyo.
(Picha na Bashir Nkoromo)
No comments:
Post a Comment