Monday, October 07, 2013

HAPPY BIRTHADAY MH JAKAYA MRISHO KIKWETE


SALAMU NA DUA YA SIKU YA KUZALIWA KWAKO MH RAIS WA TANZANIA JAKAYA MRISHO KIKWETE .

SIKU YA KUZALIWA (BIRTHDAY) KIMTAZAMO NI SIKU YA FURAHA SANA KWA MWENYE KUKUMBUKA SIKU YAKE HIYO YA KUZALIWA.

LAKINI HUYO MWENYE KUKUMBUKA SIKU HIYO NA WENYE KUMTAKIA KHERI YA KUKUMBUKA SIKU HIYO YA KUZALIWA IKIWA WOTE WAPO HAI TUNAPASWA KUZINGATIA YA KUKUMBUSHANA YAFUATAYO :-


1.Miaka Inasonga Mbele . Umri una Pungua na siku za Kuishi Duniani nazo zinapungua.


2.Dunia ni Shamba la kuitengeneza Vyema Mtu Akhera yako hatuna Budi kuombeana na kukumbushana zaidi katika kuvuna na Kuandaa zawadi ya kwenda nayo huko kwa Ukumbusho ulio na Busara na hekma ndani yake.


3.Kumshukuru M/Mungu na Wazazi kila wakati na Kila siku hasa unapokuwa una kumbuka Siku yako ya kuzaliwa Kwa Neema ya Uhai ulio nao na Wazazi kuwa Ni Sababu ya kuwepo kwako katika Dunia.


4.Kuombeana Maisha Marefu/Mafupi ya Ibada na kufa katika Njia ambayo M/Mungu anairidhia.


IKIWA KAMA ATAKUWA AMEKUFA NA MKAWA MNAENDELEA KUKUMBUKA NA KUMKUMBUKA KUPITIA SIKU YAKE YA KUZALIWA KUBWA AMBALO NYINYI MLIO KUWA HAI NI KUMUOMBEA DUA NA KUENZI YALE MEMA ALIYO YANZISHA NA KUYAACHA DUNIANI.


UNAPO KUFA MWANAADAMU MAMBO YAKO YOTE YANA KWISHA KITABU CHAKO KINAFUNGWA UTABAKI UTAJO WA MEMA YAKO KATIKA ELIMU NA FIKRA ZAKO KATIKA MAENDELEO YA WAISLAM NA JAMII YOTE KWA UJUMLA.


M/MUNGU AKUPE MAISHA MAREFU YA IBADA , SUBRA , UVUMILIVU NA UJASIRI WA KUPATIA KWA UWEZO WAKE M/MUNGU KATIKA UONGOZI WAKO WA NCHI NA JAMII KWA UJUMLA. HAPPY BIRTHDAY , HAPPYBIRTHDAY , HAPPY BIRTHDAY .


NAWASHUKURU SANA KWA KUWA PAMOJA NAMI KATIKA HILI NA LENGINE MUNGU AWABARIKI NA ATUBARIKI SOTE KWA UJUMLA NA ATUPE UPENDO WA DHATI NA MWISHO MWEMA . AMIIN


ADMIN WA KIJANA WA KIISLAM DSM.

GHALIB N. A . MONERO KITIYAGWA.

No comments:

Post a Comment