Tuesday, October 15, 2013

MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA JENGO LA HUDUMA YA MAMA NA MTOTO HOSPITALI YA RUFAA IRINGA.

Mke  wa rais mama  Salma  Kikwete kulia akizungumza  jambo na mkuu wa mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma leo kabla ya kuzinfua  jengo la huduma ya  wanawake na  watoto katika Hospital ya  Rufaa ya mkoa  wa Iringa
Mfanyabiashara  Salim Asas Abri katikati  ambae ni mmoja kati ya  wadau  wakubwa wa uchangiaji wa maendeleo ya  mkoa  wa Irionga akiwa katika  ufunguzi  wa  jengo hilo
 
Wadau wa maendeleo mkoa  wa  Iringa wakisikiliza  hotuba ya mke wa Rais
 
 
Na  Francis Godwin Blog
MKE wa  Rais  mama  salma Kikwete  amezindua  wodi  la  kisasa la  huduma  ya  wanawake na  watoto  katika  Hospital  ya  Rufaa ya  mkoa  wa  Iringa  huku  akipongeza  jitihada  kubwa  zilizofanyika katika Hospital  hiyo katika  kuboresha  huduma ya mama na mtoto.
Mbali  ya  kuzindua  jengo  hilo bado  mama  Salma  Kikwete  amewashukia  wakazi wa  mkoa  wa Iringa  ambao  wanaendelea kuongeza kasi ya maambukizi ya  virusi  vya  UKIMWI kwa  kusaliti  ndoa zao na kuwataka kuacha mara  moja.
Akifungua  wodi  hilo leo Mama Kikwete  alisema  kuwa  serikali  imelenga  kuendelea  kuboresha  huduma ya  afya na kuwa mbali ya kuboresha majengo bado  serikali imeendelea  kuboresha  elimu ya  watoa huduma  kama njia ya kuboresha  zaidi  huduma ya afya.
Hata  hivyo alisema changamoto za madawa na  madaktari  serikali itaendelea kushughulika  na  kuwataka  wanawake  kuendelea  kutumia majengo  hayo na kuepuka  kuwapeleka  watoto  kwa waganga  wa kienyeji ama  wao  kujifungulia majumbani .
Kwani  alisema  kukamilika na kuboreshwa  kwa  huduma  hizo ni  kuepusha  wazazi na watoto   kuendelea  kuwa na fikra  potofu  kuwa  watoto wao wamelogwa  pindi  wanapokosa  huku  wakiacha  kufika hospital na badala  yake  kwenda kwa  waganga  wa jadi.
Katika  hatua  nyingine  aliwataka  viongozi na wananchi wa  mkoa  wa Iringa  kuendelea  kuyatunza majengo  hayo ambayo  yamejengwa kwa  fedha za wahisani .
“ kumekuwa na tabia ya  baadhi ya  wananchi  kuhujumu miundo  mbinu ya  serikali kwa  kuiba  vifaa mbali mbali kwa madai  kuwa ni mali ya  serikali …..hili  si jambo  jema  lazima  wote  tushirikiane  katika  vifaa hivyo ambavyo ni mali ya watanzania wote”
Mama  Kikwete  amesema  kuwa  kwa upande  wake  ataendelea  kutoa  ushirikiano kwa  Hospital  hiyo katika  kutatua  changamoto mbali mbali  ikiwemo ya ushauri na kufikisha changamoto hizo sehemu  husika.
Japo  alisema  kuwa  suala la uhaba wa  madaktari  serikali ni suala  ambalo  tayari  serikali  imeanza  kulifanyia kazi  ni pamoja na  kuendelea  kuongeza madaktari  katika  kuwapa mafunzo madaktari  wapya  ambao  wataweza  kuongezwa katika Hospital  hapa  nchini.
Alisema  kuwa maambukizi ya  UKIMWI  Iringa ni asilimia  9.1 ambapo  ni  sawa na  watu  9 kati  ya 100 mkoani Iringa  wameathirika  idadi ambayo ni kubwa  kuliko ile ya  taifa  ya wastani  wa  watu  5  ambao  wameathirika  hivyo  mkoa  wa Iringa bado  upo  juu kwa maambukizi hayo.
“  Watu  wa  Iringa  ari  zaidi nguvu  zaidi mmeiwaka  katika  maambukizi ya UKIMWI hivyo nawaombeni   sana  watu wa Iringa  kujilinda  zaidi  na  kuepuka  kusaliti ndoa  zenu  na  wale ambao bado kuona ama kuolewa  basi  kujiheshimu  zaidi”
Pia  aliwataka  wananchi  wa mkoa  wa Iringa  kujenga  utamaduni  wa kupima  afya  zao mara  kwa mara  na  wale  ambao  watabainika  wameathirika  wasisite  kutumia  dawa  za  kufubaza  virusi  vya UKIMWI  na  kuachana na tabia ya  kuacha  matumizi ya  dawa  hizo.
Huku  wale ambao  bado hawajaambukizwa  basi kutulia  na  kujilinda  ili wasipate  maambukizi hayo na  kuwaomba  wanawake  wajawazito  ambao  watakubwa na maambukizi ya VVU  basi  kufika Hospital na kupima ili  kuwezesha  watoto kuzaliwa bila maambukizi.
Wakati  huo  huo mama  Kikwete  aliwataka  wanaume ambao bado kupatiwa  huduma ya  Tohara  kujitokeza  kufanyiwa  huduma   hiyo  ili  kusaidia  kupunguza  maambukizi ya VVU.

No comments:

Post a Comment