Katibu Mkuu wa sasa wa CCM, Abdulrahman Kinana, akisalimiana na Katibu
Mkuu mstaafu Willson Mukama, walipokutana kwenye Mkutano wa sita wa
Makatibu Wakuu wa vyama vilivyokuwa vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, leo
katika hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa
NEC, Oganaizesheni CCM, Mohamed Seif Khatib
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahmani Kinana akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa
Chama Cha FRELIMO cha Msumbiji, Philipe Paunde wakati wa mkutano huo
Katibu Mkuu wa chama cha ZANU-PF cha Zimbabwe, Dydmus Mutasa akiwa kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Wilson Mukama akisalimiana na Dk. Asha-Rose Migiro wakati wa mkutano huo.
Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Kikomunisti cha
Jamhuri ya Watu wa China, Ai Ping, wakati wa mkutano huo
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Ai Ping wa chama cha CPC
cha china wakati wa mkutano huo. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM
(zanzibar), Vuai Ali Vuai
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwaelekeza jambo, Katibu wa
NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Katibu
wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wakati wa mkutano huo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza kabla ya kuanza kwa kikao hicho
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akifungua mkutano wa
sita wa Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa
Afrika, leo kwenye hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam. Kushoto ni
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro
na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
Mkutano huo ukiendelea katika hoteli ya Kunduchi Beach
Mwenyekiti wa Mkutano wa Sita wa Vyama vilivyokuwa vya Ukombozi Kusini
mwa Afrika, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiendesha mkutano
huo, leo katika hoteli ya Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar Vuai Ali Vuai na kulia ni Katibu
wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro.
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mkutano huo
VIONGOZI wa vyama vilivyokuwa vya Ukombozi Kusini mwa Afrika,
walioshiriki kwenye mkutano wa sita wa vyama hivyo, leo kwenye hoteli ua
Kunduchi Beach, jijini Dar es Salaam, Kutoka kushoto, Katibu Mkuu wa
Chama Cha ANC cha Afrika Kusini, Gwede Mantash, Katibu Mkuu wa chama cha
ZANU-PF cha Zimbabwe, Didy Mutasa, Naibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa wa Chana Cha Kikomunisti cha China, Ai Ping,Katibu Mkuu wa
MPLA cha Angola, Julio Paulo. Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana,
Katibu Mkuu wa chama cha FRELIMO cha Msubiji, Philipe Paunde na Katibu
Mkuu wa Chama cha SWAPO cha Namibia,Nangolo Mbumba
Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika,
wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine waandamizi, baada ya
ufunguzi wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Chama Cha ZANU-PF, Didy Mutasa akionyesha alama ya hamasa
ya chama chake, alipozungumza na waandishi wa habari, wakati wa mkutano
wa makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi mwa kusini mwa
Afrika, kwenye hoteli ya Kunduchi Beach, Dar es Salaam. Kushoto ni
Katibu Mkuu wa CCM, Andulrahman Kinana na Wanne kushoto ni Katibu wa
NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
No comments:
Post a Comment