Friday, October 18, 2013

NASAHA

Nasaha kwangu na Kwa Ndugu zangu Vijana wengi tuna Jazba za Kueleza Jambo au Mambo ya Ki elimu Pasina Dalili na Mambo yanapo kuwa na Tofauti za Wanachuoni wengi wetu huwa Tunafumbia Macho kujua Upande Mwengine wa Wanachuoni wamesemaje na Kubaki na Msimamo Mmoja pasina haja ya kutaka kujua Upande Mwengine hili ni Jambo zuri lakini litazidi Uzuri ikiwa utapania kutaka kujua Dalili za Pande zote ili kila litakapo semwa Jambo unakuwa Unajua ameegemea Upande Gani na Kwa dalili gani ...

NASAHA HIZI SAANA KWA VIJANA AMBAO TUNAANZA KUTAMBAA KATIKA MAMBO YA UTAMBUZI WA ELIMU NAWASHUKURU SANA KWA KUFAHAMU LENGO LANGU.
--------------------------------------------------------
Tipps : Ndugu yangu Mpendwa Jua kuwa Masheikh na Vijana wengi wa Afrika Mashariki wa Ki - Waislamu Mafundisho ya Ibada wanachukua kutoka katika Chuo / Madh - hab ya Muhammad bin Idrissa Shafiih (Imamu Shafiih) ili upate kujadiliana Vizuri na Wazee na Vijana wengi walio lelewa na Wazee Chukua Nasaha zangu Ewe Kijana Msome Imamu vizuri Imamu Shafiih na Walio mfata Imamu katika Elimu ya Fiqh ukisha ielewa Vyema Naaqishi ( Dabate ) kwa Adabu za Ki elimu na Elimu yako itazidi , SI VYEMA KUITANA MAJINA MABAYA NA KUTOANA KWA DINI KATIKA MAMBO YENYE TOFAUTI NAWASHUKURU KWA KUNISOMA NA KUNIFAHAMU.

No comments:

Post a Comment