Ewe Ndugu yangu katika Imani kama tulivyotangulia sema kuwa Inshallah Mara hii
tutaangalia AINA ZA JOSHO/KUKOGA , MAMBO YANAYOWAJIBISHA KUKOGA inshaAllah Tuanze Kuangalia.
AINA ZA JOSHO
Kuna Aina Mbili za Josho/Kukoga kwa Mtazamo wa FiQh
1.Faradhi/Wajib
2.Sunna
JOSHO LA FARADHI
Josho la Faradhi Ni Josho amabalo haitosihi Ibada yenye Kuitaji Twahara Mfano wa Swala Mpaka kukoga kwanza Pindi pale kutakapo kuwepo Sababu zake hilo Josho la Faradhi.
SABABU ZA JOSHO LA FARADHI/WAJIB
Sababu ambazo zinamfanya Mtu akoge Josho la Faradhi Ni Kama zifuatazo :-
1.Janaba.
2.Hedhi/Nifasi.
3.Kujifungua
4.Mauti
Haya Ndio Mambo ambayo yakimpata Muislam anatakiwa akoge Josho la Faradhi/Wajib.
Tuangalie Moja katika Mambo hayo Manne kwa Undani Japo Kidogo.
JANABA
Neno janaba linachukua maana ya MANII yatokayo kwa mchupo.
Tunaposema fulani ni mwenye janaba/ana janaba tunamaanisha si mwenye Twahara/hana Twahara kutokana na kutokwa na manii au kujamiiana yaani kutokana na kufanya tendo la ndoa.
MAMBO YASABABISHAYO JANABA :
Janaba husababishwa na mambo mawili
1.Mwanamume/Mwanamke kutokwa na manii.
2.Jimai
Njia Ambazo Mtu huweza kutokwa na Manii.
1.Kuota Usingizini kama anafanya Tendo la Ndoa
2.Kutoka Kwa Kuchezeana na kushikana shikana Baina ya Mwanamke na Mwanaume.
3.Kutoka kwa Athari za Kutazama/Kufikiri kuliko athiri Moyo N.k
2.Jimai
Katika Mambo ambayo yanasababisha Janaba ni Jimai Kwa Maana kujamiiana hata kama manii hayakutoka.
Mwanamume akiingiza sehemu tu ya Dhakari yake katika tupu ya mwanamke basi imewapasa wawili hao; mwanamume na mwanamke huyo kukoga josho la kisharia bila ya kuangalia wametokwa na manii au laa.
Kinachozingatiwa hapa ni muingiliano na mvaano wa tupu mbili hizo ya Mwanamume na Mwanamke na si utokaji wa manii.
Dalili.
Imepokelewa na Abu Hurayra Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake kutoka kwa Mtume (S.A.w) amesema : " Mwanamume akikaa baina ya mapaja na miundi yake (mwanamke), halafu akamuendesha mbio, hakika limekwishapasa josho" kama alivyosema Mtume Bukhari na Muslim.
Na katika upokezi wa Imaam Muslim kuna ziada " Hata kama hakutokwa na manii". Kama alivyosema Mtume.
Maana ya Manii kwa Pande Zote Mbili Mwanaume na Mwanamke Manii kwa upande wa mwanamume ni maji Meupe, mazito yachupayo ambayo hutoka wakati anapofikia kilele cha matamanio ( Hutoka kwa Ladhaa Utamu ).
Manii Upande wa Mwanamke ni maji ya manjano na ni mepesi.
Ziko Hadithi Nyingi Zinazo tolea dalili kuwa utokaji wa manii huwajibisha josho Miongoni Mwazo ni Imepokelewa na Ummu Salama M/Mungu amuwie radhi amesema : Ummu Sulaym alikuja kwa Mtume (S.A.W) Akasema : Ewe Mtume wa M/Mungu, bila shaka M/Mungu haoni haya kusema haki, jee, inampasa mwanamke kuoga atakapo ota ? Mtume akajibu : " Naam , atakapo yaona maji (manii)" Kama alivyosema Mtume Bukhari na Muslim.
No comments:
Post a Comment