Tuesday, June 05, 2012

MAANA YA JOSHO





Asalaam Alaykum Ndugu zangu katika Imani leo kwa Uwezo wake M/Mungu Tupo katika Kuangalia Maudhui Mpya Katika Mlango huu huu wa Twahara ambao Tumeuanza Mawiki yaliyopita InshaAllah Tuendelea Kujikumbusha Machache ambayo yanahusu Josho/Kukoga kwa Kadri M/Mungu atakavyo tuwezesha Tuanze Kuangalia Maana ya JOSHO/KUKOGA katika Sharia.

MAANA YA JOSHO

Josho kisharia ni kitendo cha kuyapitisha/Sambaza maji mwili mzima kwa nia maalum.

HUKUMU NA DALILI YA JOSHO
Josho kisharia ni WAJIBU/FARDHI kwa Kila Muislam pale atakapo patwa na Moja katika Mambo ambayo yanamlazimu Kukoga Mfano Janaba,hedhi na Nifasi.

Dalili ya Kupasa Kukoga/Josho Qur an Sunna
Dalili ya Kwanza Qur an .
M/Mungu Mtukufu anasema "NA MKIWA NA JANABA BASI OGENI" Qur an Suratul Maidah Aya ya 6.
Na amesema tena katika Aya Nyengine "NA WANAKUULIZA JUU YA HEDHI; WAAMBIE HUO NI UCHAFU. BASI JITENGENI NA WANAWAKE WAKATI WA HEDHI ( Siku zao ). WALA MSIWAKARIBIE MPAKA WATWAHIRIKE" Qur an Suratul - Baqara aya ya 222.

Dalili katika Sunna
hadithi iliyopopkelewa na Abu Hurayra Radhi za M/Mungu Zimshukie Juu yake amesema, Amesema Mtume wa M/Mungu rehma za Mungu zimshukie Juu yake na Amani "Ni haki ya kila muislam kukoga siku moja katika jumaa, akaosha kichwa na mwili wake" Bukhari na Muslim.

HEKMA YA KUKOGA/JOSHO.

1.Kupata Thawabu
Kwa sababu josho kwa maana na mtazamo wa kisharia ni IBADA kwa kuwa ndani yake kuna kutekeleza amri ya sharia na kuitumia hukumu ya sharia Kwa hivyo kwa utekelezaji huu wa amri na hukumu ya sharia Mja hupata ujira Mkubwa kwa Mola wake.
Rejea Hadith ya Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) Anasema "Twahara ni nusu ya imani" Kama alivyosema Mtume Imepolewa Hadith na Imamu Muslim.
kwa Mujibu wa Hdithi hiyo Ni vyema ikaeleweka kuwa Twahara imekusanya Udhu, Josho, Tayamam Na N.k.

2.Kuwa Msafi Muislam anapokoga mwili wake hutakasika na kuwa msafi. Usafi huu ni kinga kubwa ya vijidudu vinavyoweza kusababisha maradhi kama vile upele na N.k.

3.Kuwa Mchangamfu na kupata nguvu Mpya.

Hizi ni katika Hekma za Chache za Kukoga/Josho ama Kwa Ujumla tunaweza sema kuwa falsafa ya josho Twahara vitu hivi humuandaa Mtu/Mja na kumuweka katika nafasi nzuri ya kuwasiliana na kuzungumza na Mola Muumba/Mola wake ndani ya swala akiwa katika hali njema kabisa.

InshaAllah Post Ijayo Tutaangalia AINA ZA JOSHO Mambo ambayo yanamuwajibisha Mtu kukoga na Ukamilifu wa Kukoga M/Mungu Ndiye Mjuzi

No comments:

Post a Comment