Monday, June 04, 2012

DINI YA KIISLAM


Ewe Kijana Mwenzangu wa Kiislam tukumbuke kwamba Dini yetu ya Kiislam Ni dini iliyotimia na kukamilika katika kila Nyanja MISINGI MIKUU YA KUUFAHAMU USLAMU UKAMILIFU WAKE NI QUR AN NA HADITH (Wamekubaliana Wana wachuoni wote ) na ipo Misingi Mingine Wametofautiana Wanachuoni katika Matawi na wala Si Misingi au Nguzo ambazo zinaujenga Uslam Inshallah Tuendelee kuwa Pamoja kwa Uwezo wake Allah tutafanya Muendelezo wa kukumbushana katika Moja moja yahusuyo Dini yetu ya Kiislam.
DALILI YA KUWA DINI YA KIISLAM IMEKAMILI M/Mungu anasema:
Leo walio kufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini.QUR AN Surat Al-Maidah Aya ya 3.
M/MUNGU amesema kweli.
Hivyo kaka yangu Mpendwa Dada yangu Mpendwa Kijana Mwenzangu katika Uislam Jambo lolote ambalo litakuwa linakuzongwa na kutolifahamu fuata Maelekezo ya Aya Ifuatayo katika Surat An - Nahl Aya ya 43 Mungu anasema : Waulizeni wenye ukumbusho (Elimu/Ujuzi/Utambuzi) kama nyinyi hamjui.
Nawatakia siku Njema na kazi Njema Wenu katika Udugu wa Kiimani

No comments:

Post a Comment