Monday, June 04, 2012

QASWIDA


Illahi tupe Mahaba ya kumpenda Nabia.
Thuma na Aqarabah na Swahaba wote pia.
Tufungulie ya ijaba ya Akhera na Dunia.
Uturuzuku Jalia mahaba ya Mtume wetu.
Fungamano la Moyoni mola wetu Wadudu.
Mwengine hatumuoni ila wewe ya Wahidu.
Tumiminie Nyoyoni mahaba ya kukuabudu.
Mola wetu ya wahidu tunusuru ya Allahu.
Yaaillah Dua zetu kwako hazitunufaishi.
wala kukuasi kwetu kabisa hakukudhulishi. 
Tufutie Dhambi zetu Rehma zako hazishi. 
Katika mema tuishi tusamehe Mola wetu.
Linukishe Vyema Ya illahi Mola Raufu. 
Kaburi la Bwana lizidishie Harufu.
kila kinukacho uzuri na utukufu. 
Hizo ni Rehema na Salamu na Amani Kwa Tumwa Karima
Alhabib Ally Mzee Comorian - Ahabab Rasul Kariakoo

No comments:

Post a Comment