Tuesday, June 05, 2012





Ewe Ndugu yangu katika Imani Inshallah kwa uwezo wake Allah tunahitimisha Ukumbusho wetu wa Mlango wa Najisi na jinsi ya kutwaharisha kwake kwa kumalizia vitu vya aina Mbili ambavyo ukumbusho uliopita hatukuviongelea nanvyo ni
SAMLI, JIBINI, SIAGI NA MFANO WA VITU HIVYO PAMOJA JINSI YA KUITWAHARISHA NGOZI.

1.SAMLI, JIBINI, SIAGI NA MFANO WA VITU HIVYO

Samli, jibini siagi na vitu vinavyofanana navyo vikiingiwa na najisi na vikiwa katika hali ya ugumu yaani vimeganda na haviko katika hali ya kumiminika,
hutwahirika kwa kuitoa najisi iliyoingia pamoja na sehemu zinazozunguka zilizo jirani na najisi ile.

Bwana Mtume Rehma za M/Mungu zimshukie juu yake na Amani aliulizwa kuhusiana na (hukmu ya) panya aliyetumbukia (na kufia) ndani ya samli, akajibu "Mtupeni na sehemu inayomzunguka na kuleni samli yenu". kama alivyosema Mtume Imepokewa Imamu Bukhar
Ewe Ndugu yangu katika Imani ama ikiwa Samli, Siagi, Jibini na chochote chenye kufanana navyo katika hali ya kumiminika/maji maji na ikaingiwa na najisi ita najisika yote na haitofaa tena kwa matumizi ya binadamu.


2.TWAHARA YA NGOZI

Ngozi ya mnyama hutwahirishwa kwa kudibaghiwa.
Dabgh ni kuondosha damu, mafuta na mabaki ya nyama zilizosalia katika ngozi baada ya mnyama kuchunwa.
Uondoshaji huu hufanyika kwa kutumia vitu vikali vyenye muonjo wa asidi au Jivu, baada ya hapo ndipo ngozi hutwahirishwa na maji na kufaa kutumika kwa matumizi mbali mbali ya binadamu.
Imepokelewa na Ibn Abbas – Mungu amuwie Radhii Bwana Mtume (S.A.W) Amesema "Ngozi itakapo dibaghiwa imetwahirika" kama alivyosema Mtume Imepokewa Hadith na Maimamu wawili Bukhaar na Muslim.
TANBIHI
Haitwahariki Ngozi ya Nguruwe,Mbwa na viwili vinavyo zaliwa na wawili hao
Hapo InshaAllah Tutakuwa tumemaliza/tumehitimisha ukumbusho wetu inshallah tujiandae na Maudhui Mpya

No comments:

Post a Comment