Ewe Ndugu yangu katika Imani Kijana Mwenzangu M/Mungu anasema :-
Na (yeyote) atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.
Aseme:(huyo mtu atakae fufuliwa kipofu) Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona
umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona?(Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo
hivyo. Zilikufikia ishara(Aya) zetu, nawe ukazisahau; na kadhaalika(vilevile) leo unasahauliwa.
Qur an Surat Taha Aya 124 Mpaka 126.
Subhana Allah
Takafakarii Ndugu yangu Natambua kwamba kuwa mbali na Allah hata kama utakuwa Taajiri Milionea basi utakuwa bado upo katika Maisha ya Dhiki na Mwisho wake kama Qur an ilivyoeleza Mungu tusaidie waja wako tusiwe mbali na Maamrisho yako.
Hii picha nimeipata katika moja ya website ambapo walikuwa wakieleza Utukufu wa Qur an Wadudu wameweza tafuna pembeni ya Ma s hafu na wameheshimu kuyafikia maneno yake Allah Subhanahu wa Taa3la.
Ndugu zangu tujitahidi tusiihame Qur an kiasi hiki
No comments:
Post a Comment