Ewe
Kijana Mwenzangu katika Kumbusho Muhimu sana Ni zote zilizopita na hii
tuifanyie kazi Mungu Tusaidie na tupe uwezo katika kutekeleza Maamrisho
yako Amiin
Ukumbusho wa leo Unahusu Kustanji.
Maana yake
Kustanji/Kuchamba ni kusafisha na kuondoa najisi iliyotoka katika mojawapo ya tupu mbili Mbele au Nyuma ya Mwanaadamu.
Kustanji/Kuchamba baada ya kukidhi haja ni WAJIBU/FARADHI kama tutakavyoona katika kauli za Mtume Muhammad Rehma za M/Mungu zimshukie juu yake na amani.
Ina faa Kustanji kwa kutumia Maji Mutlaq(maji halisi) ambayo ndiyo asili katika kujitwahirisha na najisi.
Inajuzu pale panapokuwa hakuna Maji kutumia vitu vyenye Sifa zifuatazo:-
1.Kigumu Mf wa Jiwe.
2.Chenye Kuparuza (kisichoteleza)
3.Kinachoweza kuondosha najisi.
Kumbuka kwamba katika vyote hivyo ni bora kutumia Maji na kama uko na vyote viliwili uanze kisichokuwa Maji kisha umalizie na Maji kwani Huondosha Najisi yote kinyume na Vingine.
Ni haramu kustanji kwa kilicho chakula cha binadamu kama vile mkate au chakula cha majini kama vile mifupa. Amesema Bwana Mtume Rehma za Mungu zimshukie Juu yake na amani Amesema " Msistanji kwa (kutumia) kinyesi cha wanyama wala mifupa kwani hiyo (mifupa) ni chakula cha ndugu zenu majini" kama alivyosema Mtume Imepokelewa hadith na Tirmidhiy.
ADABU/TARATIBU ZENYE KUFUNGAMANA NA UINGIAJI NA UTOKAJI MAHALA PA KUKIDHI HAJA
Ni Vema kwa mwenye kutaka kukidhi haja, atangulize mguu wake wa kushoto wakati wa kuingia chooni na mguu wa kulia wakati wa kutoka chooni, kama tulivyofundishwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu. Kadhalika asiingie na chochote chenye jina la Mwenyezi Mungu au jina lolote tukufu kama vile jina la Mtume au aya ya Qurani Tukufu. Bali imemlazimu muislamu kukivua kitu hicho wakati wa kuingia chooni. Pia imesuniwa kuleta dua wakati wa kuingia chooni. Pia imesuniwa kuleta dua zilizothibiti kutoka kwa Bwana Mtume kabla na baada ya kutoka chooni.
Aseme anapoingia Chooni
BISMILLAH ALLAHUMMA INNIY AUDHUBIKA MINAL KHUBUTHI WAL-KHABAITH.
Na anapotoka aseme :-
aseme
GHUFRAANAKA AL-HAMDU LILLAHIL-LADHIY ADH-HABA ANNIYL-ADHA WA-A’AFANIY.
ADABU/TARATIBU ZINAZOFUNGAMANA NA MAHALA PA KUKIDHIA HAJA
1.Njia ya watu au mahala wanapokaa, hii ni kutokana na kero na maudhi yatakayowapata.
2.Tundu iliyopo ardhini au ufa wa ukuta/kiambaza. Hii ni kwa sababu ya kumlinda na kumuepusha mkidhi haja na madhara yanayoweza kumpata. Kwani anaweza akawamo ndani ya shimo/ufa mdudu mwenye kudhuru kama vile nge au nyoka, huyu akakerwa na haja akaamua kumtokea mtu na kumdhuru
3.Chini ya mti utoao matunda.
Hii ni kwa ajili ya kuyahifadhi na kuyalinda matunda yado ndokayo yasipatwe na najisi.
Ni mamoja ikiwa matunda hayo yanaliwa au hayaliwi lakini yana manufaa mengine kama dawa.Na Miti ya Kivuli kwa ajili ya Mapumziko ya watu kwa uchovu na ukali wa jua.
4.Maji yaliyotuama (yasiokwenda). Hii ni kutokana na kichefuchefu watumiaji wa maji hayo yakiwa ni mengi yasiyoharibika na najisi na kuyanajisi yakiwa machache na hivyo kuyafanya yasifae kutumika.
Imekuwa ni kawaida kwa watu kukidhi haja sehemu yeyote bila ya kuchunga Adabu hizi huenda tulikuwa hatufahamu Leo Inshallah tumefahamu tujilinde ndugu zangu na Najisi na tuzilinde sehemu zetu katika kuweka Mazingira Safi Uislam Ni Usafi Ni aibu na haifai kwa Muislam kwenda kinyume na Misingi ya Mafundisho yako.M/Mungu ndiye Mjuzi zaidi Inshallah Mungu akipenda tutaendelea ...

No comments:
Post a Comment