Tuesday, June 05, 2012

UDHU




Ndugu yangu katika Imani Kaka yangu Mpendwa Dada yangu Mpendwa leo Inshallah kwa Uwezo wake M/Mungu Mtukufu tunaingia katika Ukumbusho Mpya Niwaombe wale Marafiki zetu na Ndugu zetu wageni warejee katika Post zetu zilizotangulia ili tupate kwenda sawa.Ukumbusho wetu leo utahusu au zungumzia Udhu na Kama Ada yetu tunaangalia neno kwa Maana Mbili ya Lugha na Maana ya watu Sharia(Fiqh).

1.MAANA YA UDHU

Tamko/Neno udhu linafasirika katika lugha ya kiarabu kama wema, uzuri na ung'avu.
Ama maana ya udhu katika istilahi ya wanazuoni wa fani hii ya Elimu ya Sharia (Fiqh) Udhu ni twahara inayotumia maji, twahara hii inahusisha viungo maalum vya mwili, baadhi yake hukoshwa kama mikono, uso na miguu na vingine hupakwa maji kama vile kichwa.

2.HUKUMU YA UDHU NA DALILI YAKE
Udhu kwa maana tulivyoieleza ni FARDHI/WAJIBU katika kusihi na kukubalika kwa ibada ya swala kwani hapana swala bila ya udhu kwa maneno mengine, tunaweza sema kuwa udhu ndio msingi mkuu na imara wa ibada ya swala.
Udhu ndani ya Qur-ani unapatikana katika kauli ya Mwenyezi Mungu aliposema :
"Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Swala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni..." Qur an Suratil Maidah aya ya 6

Ama dalili na ushahidi wa udhu katika sunna ni ile kauli yake Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehma za M/MUNGU zimshukie Juu yake na amani aliposema " Allah haikubali swala ya mmoja wenu atakapohuduthi kwa Maana kwamba atakapo tengukiwa na udhu mpaka atawadhe (tena)" kama alivyosema Mtume
Hadithi imepokelewa na Maimamu wawili.

3.UBORA/FADHILA ZA UDHU
Ewe Ndugu yangu Kijana Mwenzangu tukumbuke kwamba zimepokelewa hadithi nyingi kutoka kwa Bwana Mtume -Rehema za M/Mungu zimshukie juu yake na Amani katika kutaja na kuonyesha ubora na fadhila za udhu miongoni mwa hadithi hizo ni :-
Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani zimshukie juu yake "yeyote atakaye tawadha vyema ( kama alivyoelekezwa na sharia), hutoka madhambi zake mwilini mpaka chini ya kucha zake"kama alivyosema Bwana
Mtume Muslim.
Na katika Hadithi Nyengine Mtume (S.A.W)
amesema "Hakika umati wangu wataitwa siku ya Kiyama (mbele ya Mola wao) hali ya kuwa wang'avu wa nyuso, mikono na miguu kutokana na athari ya udhu, basi yeyote yule awezaye kurefusha mipaka ya viungo vyake (katika kutawadha) na afanye hivyo." kama alivyosema Mtume Imepokelewa Hadith na Imamu Muslim.

Ewe Ndugu yangu Mpendwa baada ya kujua haya
Inshallah azimia na tia Nia kuanzia sasa kushikamana na Udhu ili zisikupite fadhila na Ubora wa Udhu kama tulivyo eleza Inshallah tuwe pamoja katika Ukumbusho Ujao ambao tutaeleza Namna ya kutawadha.

No comments:

Post a Comment