Monday, June 04, 2012

MAANA YA FIQH NA MISINGI YAKE


Ewe Ndugu katika Imani Kijana Mwenzangu Baada ya kuitaja Misingi Mikuu Mitatu ya Dini Ambayo Ni 1.UISLAM 
2.IMANI 
3.IHSAN 

Na  kueleza Maana ya Nguzo ya kwanza katika Nguzo za Uislam Ambayo Ni Shahada MBILI Inshallah leo tunaendelea na Safari yetu kwa Kueleza Maana ya neno FIQH Kilugha na kimaana ya Wanawazuoni wa Fani hii (Shari3):

FIQH ni neno la kiarabu lenye maana mbili. Maana ya kwanza ni ya kilugha na ya pili ni ya kishari3. Katika lugha ya kiarabu neno "FIQH" maana yake kufahamu/kujua.
FIQH: kwa mtazamo wa shari3 ni fani ya elimu inyoshughulikia na kusimamia utekelezaji wa shari3, kanuni na na taratibu za Uislamu katika maisha ya kila siku kwa ujumla fiqh ni sheria zinazoyatawala maisha ya Muislamu katika nyanja zote za maisha, kuanzia elimu, ibada, uchumi, ulinzi na usalama, ndoa, mirathi N.k.

MISINGI YA FIQ-HI

Misingi ya fiq-h ni chimbuko la elimu hii yaani mahala ambamo elimu hii imechukuliwa. Elimu ya fiqh imejiegemeza katika misingi mikuu minne kama ifuatavyo:

1.Qur-ani
2. Hadithi(sunnah)
3.Ijmaa
4.Qiyaasi
Hii ndio misingi na tegemeo la elimu hii ya fiqh.
Wamekubaliana wanawachuoni wote wa Fani hii ya Elimu ya Fiqh Juu ya Misingi Mikuu Miwili yanii Qur - an na Hadith (Sunnah) Na wametofautiana katika Bakii ya Misingi Inshallah tutakuja Ona kwa wakati wake Ikiwa Bado Umri wetu wa kuishi unaendelea.

MAJINA YA MAIMAMU WAKUU WANNE KATIKA ELIMU YA FIQH 

1.IMAMU ABUU HANIFA NU3MAAN
2.IMAMU MAALIK
3.IMAMU SHAFIIH
4.IMAMU AHMAD IBN HANBAL

Inshallah Tutaendelea kueleza Maana ya kila Msingi katika hiyo Misingi Minne tulio itaja

No comments:

Post a Comment