Monday, June 04, 2012

BEGI / SANDUKU


BEGI / SANDUKU
Waislam tumehimizwa sana Upendo,ushirikiano,kutendeana mema na kila Jambo ambalo litaingiza furaha katika Nafsi ya Ndugu yako Muislam kwa Kuzingatia Misingi na Mipaka ya Dini ni Ruhsa kulitenda.
Tuliangalie BEGI / SANDUKU ni Moja katika Mambo mazuri na Mema ambayo Dada zangu na Mama zangu wa Kiislam hupenda sana kushirikiana katika hili pale Ima anapokuwa anaozesha Mtoto wake au Kujifungua Mtoto N.k.
Marafiki hutoka na kwenda kumtunza Nguo na vitu Mbalimbali amabvyo wameweza kuvikusanya kwa Ajili ya Mwenzao kwa Siku ile.
Hili ni Jambo jema sana ambalo kama Mtakuwa Mnalisimamia katika Misingi na Mipaka ya Dini tutakuwa Pamoja katika hali zote kwani ni Moja katika Njia za kuzidisha Upendo Ushirikiano N.K.
AMBAYO KWA SASA YANAYOTOKEA KATIKA JAMII YETU YA KIISLAM KUHUSU HILI SANDUKU AU BEGI NI KINYUME NA MISINGI YA DINI (NA KILA JAMBO AMBALO KWA SABABU YA JAMBO HILO KUFANYIKA HUPELEKEA KUTOKEA MAMBO AMBAYO YAKO NJE YA MISINGI YA DINI YETU LINAKUWA HALIFAI KI SHARI3 )
SINA HAJA YA KUTAJA MWANZO MPAKA MWISHO YANAYOKUWA YANATOKEA ILA SISI WENYEWE NI MASHAHIDI WA HAYA KATIKA JAMII YETU.
Waislam Tuzinduke Dada zangu/Mama zangu wapendwa katika Imani Saidianeni Kiibada ili Mpate Thawabu na Radhi za M/Mungu tuwaepushieni watoto wetu Na Ma Iblis siku ya 7 tu ya Uzawa wao kwa kuwaletea Magoma na Masherehe yasiofaa.
Tuhurumieni vizazi vyetu na Tusaidiane na kushirikiana katika kutaka Radhi za Mungu na kuitafuta ile Nafasi ya Kivuli siku ambayo hakutakua na kivuli isipokuwa Kivuli cha M/Mungu kwa wawili wenye kupendana kwa Ajili ya M/Mungu Kama Alivyosema Mtume na Ukitoa Upendo ndio unazidi Nawashukuruni

No comments:

Post a Comment