Maana ya Neno MUKALLAFU
Hili neno huenda tukawa tunalitumia sana katika safari zetu za Ukumbusho wa FIQH unapokutana na Neno hili Jee tunakuwa na kusudio gani?
Ukikutana na Neno Mukallafu hukusudiwa katika Elimu ya Fiqh ni ule umri wa Baleghe ambao atakapofika mtu Mwanamume au
Mwanamke hupata sifa ya kuwa ni mtu MUKALLAFU.
Kwa Maana kwamba anatakiwa kuyatekeleza yale yote ambayo ameamrishwa na kukatazwa na sharia Mfano Swala, Funga na ibada nyingenezo.
NI WAJIB KWA MTU MUKKALAFU KUTENDA YOTE ALIYO AMRISHWA NA KUKATAZWA NA SHARIA ILA KUACHA KWA DHARURA.
MTU MUKKALAFU AKIFANYA MEMA NA KUACHA MABAYA KWA KUTII AMRI YA MOLA WAKE HUPATA THAWABU NA AKIFANYA MABAYA HUPATA DHAMBI.
DALILI ZA BALEGHE TATU.
1.Kutimiza Umri wa Miaka 15 kwa Mwanamke na Mwanaume.
2.Kuota kwa Mwanaume na Mwanamke anapofikisha Umri wa Miaka 9.
3.Kutokwa na Damu ya Hedhi kwa Mwanamke
Hizi ndio Alama Tatu pindi anapoziona Mtu au kwa Mtoto wake anatakiwa amuhimize sana ki - Ibada kwani kila tendo lake linakuwa linazingatiwa na Kuandikwa kama Jema Thawabu na kama Baya Dhambi.
Ni vyema kuwafundisha na kuwahimiza watoto wetu Mambo mema ya Kii baada na Malezi ya Ki - Dini na kuwaeleza wanapofika Umri huu kuwa sasa Tayari washaingia katika Umri ambao Sharia ya Dini Inawazimu kwao
No comments:
Post a Comment