Tuesday, June 05, 2012





Asalaam Alaykum Ndugu zangu wapendwa nawashukuru kwa kushiriki katika Swali tulilo Uliza Jee Ingekuwa Memory zetu (Akili) za kuhifadhi Zingekuwa GB 1 Nini ungeifadhi ?

MashaAllah wengi Mmejibu Majibu Mazuri sana Nimeyapenda Sana Na kutokana na Majibu yenu nimepata Nguvu ya Kuandika Ukumbusho Ufutao.

Ewe Ndugu yangu Mpendwa Miongoni mwa Neema ambazo M/Mungu ametupa sisi Wanaadamu Ni Akili ambayo inatutofautisha na Wanyama.

Na Neema Nyengine ambayo M/Mungu ametupa ni hii Open Memory ambayo haiko na Limit GB 1 wala GB 4 iko zaidi ya GB 8 Hivyo Ndugu zangu wapendwa Kwa vile Bado tuna Pumzi na Uhai Tuanze sasa hivi kwa Ku - Format na Ku - Scan Memory zetu kwa ajili ya Kuweka Mambo Mazuri katika Memory zetu kama vile tulivyo Chagua kwa GB1 wale waliochagua QUR AN & SUNNA na Mazuri mengi Muda Bado Upo ila tusichele kusema tutafanya Kesho kwa sababu kesho huenda tusifike Tuingize Elimu na yaliyo Mazuri katika Memory zetu ili kupata fikia Malengo yetu ya Kupata Radhi za M/Mungu na Kuishi Maisha Bora hapa Duniani na Kesho Akhera.

MASHAALLAH ALHAMDULLILAH KAKA YANGU HUYOOO NA DADA YANGU NAMUONA ANAFUTA KATIKA SIMU YAKE MIZIKI NA TAARABU NA KUTAFUTA QUR AN ILI ANZE KUWEKA MAZURI KATIKA MEMORY YAKE NA YA SIMU YAKE .

MUNGU AKUBARIKI KWA KUWA MTU WA MATENDO BAADA YA KUSIKIA MUNGU AWABARIKI NYOTE KWA KUWA NAMI

No comments:

Post a Comment