Ndugu zangu Katika Imani Baada ya Kuona Vitenguzi vya Udhu Inshallah Leo kwa Uwezo wake M/Mungu tunaangalia
MAMBO YALIYO HARAMU KWA ASIYE NA UDHU
Ni haramu kisharia kwa mtu asiyekuwa na udhu kufanya mambo yafuatayo : -
1.Kuswali swala ya aina yeyote ya faradhi, au sunna au swala ya maiti Unamlazimu Udhu kwanza Ndio apate kutekeleza Ibada hizi.
Dalili.
M/Mungu anasema "ENYI MLIOAMINI ! MNAPOTAKA KUSWALI, BASI OSHENI NYUSO ZENU, …" Qur an Suratil Maidah aya ya 6.
Dalili katika Sunna.
Mtume(S.A.W) anasema " Mwenyezi Mungu haikubali swala ya mmoja wenu atakapo huduthi mpaka atawadhe (tena)" kama alivyosema Mtume hadith imepokelewa na Imamu Bukhaar.
Kumbuka Ewe kijana Mwenzangu kuwa Twahara ya hadathi ni sharti miongoni mwa sharti za kusihi Swala haitosihi Swala ila kwa kupatikana Twahara ambayo ni udhu.
2.Kutufu/kuizunguka Al-Kaaba.
3.Kuugusa Msahafu wote au baadhi yake.
Wamekubalina na kuwafikiana wanazuoni wa fani hii ya fiqh kwamba INAJUZU kwa mtu asiyekuwa na udhu kuisoma Qur-ani Tukufu bila ya KUIGUSA lakini ni Bora kwake kuwa na Udhu.
Kama alivyo ruhusiwa mtoto mdogo kuigusa bila ya udhu kwa lengo la kujifunza, kwa kuwa yeye si MTU MUKALLAF ( anayelazimiwa na hukumu za sharia).
Pamoja na ruhsa hii bado ni bora azoweshwe kuigusa Qur-an Tukufu akiwa na udhu ili kuipandikiza heshima na utukufu wa Qur-ani ndani ya moyo wake huyu kijana na achipukie akijua nini Maana ya Twahara na Ubora wake akuwe akitofautisha kati ya Qur ani na vitabu vingine.
Ndugu yangu katika Imani haya ni Machache katika tuliyojaaliwa na M/Mungu kwa Upana zaidi wa Mas alaa (Elimu hii ya Fiqh Nakushauri Kuwa Karibu Na Masheikh na Maustaadh wa Dini Ili wapate kukupa Faida zaidi M/Mungu ndiye Mjuzi zaidi

No comments:
Post a Comment