Tuesday, June 05, 2012

VITENGUZI VYA UDHU




VITENGUZI VYA UDHU

Ni mambo ambayo mojawapo miongoni mwake likimtokea/kumpata mtu mwenye udhu litasababisha kubatilika kwa udhu wake huo na kuhesabika mbele ya sharia kuwa hana Udhu.
Itampasa kuchukua Udhu tena ikiwa anataka kuyafanya yale ambayo kisharia hawezi kuyafanya Pasina Udhu.

Vitenguzi vya udhu ni vitano

1.Kutokwa na Kitu kati ya Moja ya Njia Mbili ya mbele au ya nyuma. Ni sawa sawa hicho kilichomtoka ni haja Ndogo au Kubwa au Upepo.
Dalili katika Qur an : -
M/Mungu anasema “…..AU MMOJA WENU AMETOKA CHOONI."Qur an Surat Maida Aya ya Sita,[Surat An Nisaa aya ya 43.
Maana yaani ametoka kukidhi haja yake.

Dalili katika Sunna :-
Mtume (S.A.W) “ Allah haikubali swala ya mmoja wenu atakapo huduthi ( atakapotengukwa na udhu ) mpaka atawadhe ( tena ) Mtu mmoja wa Hadharamout (Mji katika Yemen ) akasema kumuliza Abuu Hurayrah ni nini hadathi? akamjibu ni ushuzi(upepo) ".Kama alivyosema Mtume.

Madhii na Madii ni Katika Vitenguzi vya Udhu.
Rejea Somo letu katika Post za Nyuma tulipotaja Aina za Najisi.

TANBIIH : Kisia/kadiria kwa haya yaliyotangulia kila kitokacho katika tupu ya mbele au nyuma, hata ni twahara kilichotoka.

2.Kulala Usingizi Mzito hali ya kutoambatanisha Makalio katika Aridhi kiasi cha kuruhusu chochote kuweza kumtoka bila kuhisi hasa ushuzi (Upepo).
Dalili kutoka katika Sunna kauli ya Mtume – (S.A.W) “Atakayelala ( akiamka ) basi na akatawadhe” Kama alivyosema Mtume Imepokelewa na Abuu Daawoud
Ama ule usingizi mwepesi ambao mtu anakuwa anazo hisia zake na akawa amekaa mkao wa kuwambisha makalio yake katika ardhi, huu hautengui udhu kwa sababu atahisi kitakachomtoka.

3.Kuondokewa/kutokwa na akili kwa sababu ya uwendawazimu, kuzimia, kulewa ( kwa namna yoyote ile ) au kwa kutumia madawa ya kulevyaii ni kwa sababu vitu hivi huiondosha akili ya binadamu na hivyo kumfanya akose hisia za kuweza kutambua kinachomtokea.

4.Kumgusa Mwanamke(Si mtoto Mdogo) wa kando pasina kizuizi, Mwanamke wa kando ni kila Mwanamke ambaye kisharia ni halali kumuoa, hakuna uharamu baina yao ima wa Ki Nasabu/Kunyonya au Ukwe .
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu “….AU MMEWAGUSA WANAWAKE…”Qur an Suratil An Nisa aya 43

TANBIIH
Udhu hutenguka kwa Wote wawili aliyegusa na aliyeguswa.

5.Kugusa utupu wake au wa mtu mwingine hata kama ni mtoto mdogo au maiti kwa matumbo ya kiganja chake au matumbo ya vidole vyake pasina kizuizi.
Dalili juu ya hili ni kauli ya Bwana Mtume (S.A.W) “Atakayeigusa dhakari yake, basi asiswali mpaka akatawadhe (tena)”Kama alivyosema Mtume imepokelewa na Tirmidhiy.


Hivi Ndugu zangu katika Imani Ndio Vitenguzi vya Udhu naomba Nikumbushe Ukumbusho wangu Umetegemea katika FIQH YA IMAMU SHAFII yako Mambo wametofautina wanawachuoni Niwaombe tuchukue tu kama ilivyo na Inshallah Katika Safari yetu M/Mungu akitupa Umri tutaeleza Mambo yote ambayo yako na tofauti katika FIQH MUQAARANA M/Mungu ndiye Mjuzi Ndugu yenu katika Imani

No comments:

Post a Comment