Ndugu zangu wapendwa katika Imani leo tena kwa uwezo wake M/Mungu Mtukufu tunarudi katika Somo la FIQH.
lakini kabla ya kuendelea Naomba nikuulize wewe kijana mwenzangu katika yale ambayo tumekwisha kumbushana kwa wiki zima hili nini umefahamu?
Kama Umefahamu naomba nijibu Maswali yafuatayo katika yale tuliyo yasoma.
1.Ngapi Nguzo za Uislam?
2.Ngapi Nguzo za Imani?
3.Ngapi Nguzo ya Ihsani?
4.Nini Maana ya Fiqh?
5.Misingi ya Fiqh Ni Mingapi?
6.Hukmu za Sheria3 ya Kiislam Ziko Ngapi?
7.Nini Maana ya Faradhi/Wajibu?
8.Nini Maan ya Sunna?
9.Jee Mtu akifanya Jambo ya Haramu anapata Dhambi au Thawabu?
10.Tumesema kuwa Jambo Mubaha ukilifanya hupati Thawabu wala dhambi lakini tufanya Uzinduzi au Angalizo tukataja hali fulani katika Jambo la Mubaha ukilifanya unapata Thawabu Naomba nikumbushe jambo hilo ni jambo gani?
Nawashukuruni nyote ambao Mtashiriki katika kujibu Maswali haya niwaombe kila Mmoja achague Maswali Matano ajibu na Nikuombe Jibu lako litoke ndani ya Mlolongo wa Darsa/Ukumbusho wetu tulio kuwa tuna kumbushana kwa wiki iliyopita Nakuomba Kijana Mwenzagu shiriki katika hili Jazakum Allahu Khairan Tusisahau Kusoma Dua wakati wa kwenda Kulala Sema:
LAA ILAHA ILLA LLAH WAHDAHU LA SHARIKA LAHU LAHUL MULK WALAHUL-HAMD WAHUWA ALAA KULLI SHAY-IN QADIR.
No comments:
Post a Comment