Monday, June 04, 2012

MAJIBU YA MASWALI


Asalaam Alaykum Warahmatu llah wabarakatu yafuatayo ni Majibu ya Maswali ya Jana kwa Ufupi

1.Nguzo za Uislam ni Tano (Shahada Mbili,Swala tano , Zakkah,Funga,Kuhiji Makkah(Mwenye uwezo)

2.Nguzo za Imani Sita ( 6 ) Kumuamini Allah,Kuwaamini malaika wa Allah,Kuviamini vitabu vya Allah,Kuwaamini mitume (wote ) wa Allah, Kuamini siku ya mwisho,Kuamini Qadari ya Allah (ya kheri au ya shari) kuwa inatoka kwa Allah).

3.Nguzo ya Ihsani Moja nayo ni Kumuabudu Allah kama unamuona Kama humuoni yeye anakuona wewe.
4.Maana ya Fiqh ki lugha kufahamu
Fiqh kwa mtazamo wa sheria ni fani ya elimu inyoshughulikia na kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni na na taratibu za Uislamu katika maisha ya kila siku kwa ujumla fiq-hi ni sheria zinazoyatawala maisha ya Muislamu katika nyanja zote za maisha, kuanzia elimu, ibada, uchumi, ulinzi na usalama, ndoa, mirathi N.k

5.Misingi ya Fiqh ni Minne (Qur-an,Hadithi(sunnah),Ijmaa3,na Qiyaasi.

6.Hukmu za Sheria3 ya Kiislam Ziko Tano:
Faradhi/Wajibu
Sunnah
Haramu
Mubah
Makuruuh

7.Maana ya Faradhi/Wajibu ni jambo ambalo mtu baleghe(Mukalaf), mwenye akili timamu amelazimishwa na sharia3 kulitenda. Mtu mwenye sifa hizo tulizozitaja akilitenda jambo la faradhi kama Swala, Funga n.k. kwa kumtii Mola wake hupata thawabu na akiacha kutenda bila ya udhuru(Dharura) yoyote uinayokubalika kisharia3 anakuwa anapata dhambi.

8.Maana ya Sunna kwa mtazamo wa fiqh ni kinyume cha faradhi. Kwa hivyo basi sunnah ni jambo ambalo sheria haikumlazimisha mtu kulitenda bali imempa khiyari kutenda au kutotenda. Mfano wa sunnah ni kama vile kuanza kutoa salamu, kuwapa sadaka masikini, kufunga Alhamis na Jumatatu N.k. Atakayelitenda jambo la sunnah atalipwa thawabu na atakayeacha hatopata dhambi wala kuadhibiwa ila anakuwa amepitwa na Fadhila kubwa kabisa.

9.Mtu akifanya Jambo ya Haramu anapata Dhambi.

10.Mubaha ukilifanya hupati Thawabu wala dhambi lakini Mtu akitenda jambo la Mubaah kama vile kula chakula na akatia nia ya kupata nguvu kwa ajili ya kufanya ibada, atapata thawabu na kinyume chake akinuia kwa jambo hilo hilo la Mubaah kumuasi Mwenyezi Mungu basi atapata dhambi.

Ndugu yangu katika Imani kaka yangu Mpendwa Dada yangu Mpendwa kupitia Maswali ya Jana tumeona kwamba wengi wenu Mme Like Maswali lakini Hamkujibu niwaombe basii yachukueni Majibu ya Maswali na wafundisheni Ndugu zenu na Watoto kwa wale ambao wamejaaliwa kuwa nao na kisha waulize Maswali kama tulivyo uliza Jana nawashukuruni kwa ushirikiano wenu

No comments:

Post a Comment