Asalaam Alaykum Ndugu zangu wapendwa Katika Imani Natumai Mmeamka Salama
Wengi katika Ndugu walikuwa wanataka Dua ya Kukoga Janaba Naomba Kuanzia leo Tambua kuwa hiyo iliyokuwa unaijua kwa Jina la Dua inaitwa NIA kwa Ufasaha hakuna Dua ya kukoga Janaba wala Hedhi wala Nifasi Bali huitwa Nia ya Kukoga Ima JANABA HEDHI AU NIFASI.
Na Nia Zake huwa huwa kwa Maneno yafutayo na Sehemu ya Nia ni Moyoni.
NAWAYTU RAFAAL HADATHIL AKBAR.
NAWAYTU RAFAAL JANABA.
NAWAYTU RAFAAL HEIDHI
NAWAYTU RAFAA NNIFASI
ZOTE ZIKIWA NA MAANA NANUIA KUONDOSHA JOSHO KUBWA.
ANGALIZO:
Katika Somo lilopita tulielekeza Jinsi ya Kujitwahrisha na Josho la Janaba kwa Ukamilifu wengi wanauliza Vipi ukioga kwa Bomba la Mvua au Baharini N.k
Zingatia kupatikana Mambo matatu katika hali hizo na yakipatikana hayo Twahara yako Ni sahihi.
1.NIA
2.KUONDOSHA UCHAFU.
3.KUNEA MAJI MWILI MZIMA
YAKITIMIA HAYO BASI HAKUNA TATIZO LA KUJITWAHARISHA KWA NJIA HIZO
No comments:
Post a Comment