Ndugu yangu katika Imani baada ya Kuona yale yaliyo Haramu kwa Mtu asiyekuwa na Udhu InshaAllah Tuangalie baadhi ya Hali ambazo UDHU HUSUNIWA NDANI YAKE.
1.Wakati wa kumtaja (dhukuru) Mwenyezi Mungu Mtukufu
Kumbuka Ewe Kijana Mwenzangu wa Kiislam kuwa Udhu ni silaha ya muumini ni vyema saa zote ukawa unatembea na silaha yako na hasa wakati wa kumtaja (dhukuru) M/Mungu.
2.Wakati wa kulala.
Dalili Hadithi Albaraai bin Aazib Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake amesema : Aliniambia Mtume (S.A.W) "Unapo kiendea kitanda chako (unapotaka kulala) Tawadha udhu wako wa swala kisha ulalie upande wa kulia halafu useme : ALLAHUMMA INNIY ASLAMTU NAFSIY ILAYKA, WAWAJJAHTU WAJ-HIY ILAYKA, WAFAWWADHTU AMRIY ILAYKA, WA AL JA-TU DHWAH RIY ILAYKA RAGHBATAN WA RAHBATAN ILAYKA, LAA MALJAA WALAA MANJAA MINKA ILLAA ILAYKA. ALLAHUMMA AAMANTU BIKITABIKAL-LADHIY ANZALTA, WABINABIYYIKAL-LADHIY ARSALTA." Kama alivyosema Mtume Bukhari.
3.Ni Sunna kutia udhu kabla ya kukoga josho la janaba.
4.Wakati mtu anapokuwa na Hasira sana, ni sunna akatawadhe kwa sababu udhu husaidia kuzima mchemko wa hasira na humrejesha katika hali ya utulivu.
Haya Ni baadhi ya Mambo ambayo ni Sunna Kuchukuwa Udhu kabla ya Kuyafanya yako Mengi sana Ni juu yetu Mimi na wewe Kijana wa Kiislam kuwa Karibu na Wajuzi wa Mambo ili tupate wauliza na kufahamu zaidi ya Baki ya Mambo Mengine.
Mwisho Tumalize UDHU WA MWENYE UDHURU
Tunakusudia Udhu wa watu ambao wana maradhi ambayo kwa Maradhi hayo wawezi kuhifadhi udhu wao kama wanavyoweza watu wengine katika hali ya kawaida.
Hawa ni kama wale ambao wenye Maradhi ya kutoweza kuzuia haja Ndogo (Mkojo) au mwanamke ambaye hutokwa na Damu ya Ugonywa Ukiacha Damu ya Hedhi ya kila mwezi.
Hukumu ya udhu wa watu hawa ni kwamba wanatakiwa watawadhe kila unapoingia wakati wa kila swala, wasitawadhe kabla ya kuingia wakati kwa kuwa wanatakiwa kufululiza baina ya udhu na swala.
Hii ni kwa sababu kisharia hawana udhu kwani wana hadathi ya kudumu na udhu wao ni wa ruhsa maalum waliyopewa na sharia ili waweze kuyatekeleza yale yote yasiyo tekelezeka bila ya udhu, kama vile Swala N.k
Udhu wa watu hawa utabatilika na kutenguka mara tu unapoingia wakati wa swala nyingine.
Akitaka kuswali basi itamlazimu kutawadha tena. Haya yote yanaonyesha wepesi wa sharia ya Kiislamu ambayo imejengwa juu ya misingi ya wepesi na kuondosha uzito na ugumu.
Amesema M/Mungu Mtukufu : "Wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini. Nayo ni mila ya baba yenu Ibrahim …" Qur an Surat Al - Haj Aya ya 78.
Mpaka hapo Ndugu yangu tutakuwa Tumemalize Ukumbusho wetu Kuhusu Udhu Inshallah Ukumbusho Ujao utakuwa Unahusu Jinsi Ku - Jitwaharisha na Josho Kubwa yaani Jinsi ya Kukoga Janaba NAWASHUKURUNI WOTE
No comments:
Post a Comment