Monday, June 04, 2012

UCHAMBUZI WA KILA HUKMU YA SHARIA


Ewe Ndugu yangu Mpendwa katika Imani leo Inshallah kwa uwezo wake M/Mungu tuna malizia sehemu yetu ya Mwisho katika kukumbushana 

1.Maana ya Fiqh
2.Misingi ya Fiqh
3.Faida zake
4.Hukmu ya Sharia3 katika Elimu ya Fiqh
na Mwisho kabisa Hukmu za Sharia3 ya Kiislam ambapo ndipo tuliposimamia kwa Jana na kwa kukumbushana tulizisema kuwa ni 5.

1.Faradhi/Wajibu
2.Sunnah
3.Haramu
4.Mubah
5.Makuruuh

Na leo Tunawaletea maana na ufafanuzi mdogo wa kila hukumu:-
1.FARADHI/WAJIBU

Faradhi au Wajibu ni jambo ambalo mtu baleghe(Mukalaf), mwenye akili timamu amelazimishwa na sharia3 kulitenda. Mtu mwenye sifa hizo tulizozitaja akilitenda jambo la faradhi kama Swala, Funga n.k. kwa kumtii Mola wake hupata thawabu na akiacha kutenda bila ya udhuru(Dharura) yoyote uinayokubalika kisharia3 anakuwa anapata dhambi.

2.SUNNAH

Sunna kwa mtazamo wa fiqh ni kinyume cha faradhi. Kwa hivyo basi sunnah ni jambo ambalo sheria haikumlazimisha mtu kulitenda bali imempa khiyari kutenda au kutotenda. Mfano wa sunnah ni kama vile kuanza kutoa salamu, kuwapa sadaka masikini, kufunga Alhamis na Jumatatu N.k. Atakayelitenda jambo la sunnah atalipwa thawabu na atakayeacha hatopata dhambi wala kuadhibiwa ila anakuwa amepitwa na Fadhila kubwa kabisa.

3.HARAMU

Haramu ni kila jambo ambalo sharia3 imekataza kabisa kulitenda kama vile kuiba, kusema uwongo, kunywa pombe na kadhalika. Mtu aliye baleghe na mwenye akili timamu akilitenda lililoharimishwa kwa kuvunja amri ya Mola atastahiki kupata dhambi na adhabu na akiacha kutenda haramu kwa kufuata amri ya Mola atapata thawabu.

4.MUBAAH

Mubaah ni jambo ambalo sharia3 haikulazimisha mtu kulitenda na wala haikumkataza kulitenda. Mfano wa mubaah ni kama vile kuvaa nguo nzuri mno au kula vyakula vizuri vizuri kama Biliani Pilau N.k. Mwenye kutenda jamboa la Mubaha Hapana thawabu wala dhambi ndani yake.

ANGALIZO:

Mtu akitenda jambo la Mubaah kama vile kula chakula na akatia nia ya kupata nguvu kwa ajili ya kufanya ibada, atapata thawabu na kinyume chake akinuia kwa jambo hilo hilo la Mubaah kumuasi Mwenyezi Mungu basi atapata dhambi.

5.MAKURUUH:

Makuruuh ni kila jambo ambalo linachukiza kulitenda kwa mtazamo wa sharia3. Hastahiki mtu kupata adhabu ya Mola kwa kulitenda bali akiacha atapata thawabu.

Nawashukuruni Vijana wenzangu wote ambao mpo pamoja nami Kijana Mwenzenu M/Mungu Twamuomba atupe kila yaliyo ya kheri atuzidishie ufahamu katika kutambua Hukmu na Mafundisho ya Dini yetu Nakuomba Ewe kaka yangu na Ewe Dada yangu kuwa Mjumbe kwa Mema na mazuri unayo yapata kwa Mwenzako na Familia yako kwa Ujumla na huo Ndio Upendo wa Dhati Ili tupate Fikia Lengo la kupata Radhi zake M/Mungu na kutambua Dini yetu vyema ili ipate kutuleta kuwa kitu kimoja bila ya tofauti zozote Allahu A3laam Ndugu yenu katika Imani

No comments:

Post a Comment