Ewe Kijana Mwezangu kumbuka kwamba wazazi wawili wana Thamani kubwa sana kwako na Kwangu wao ndio Sababu ya Mimi na wewe kuwepo hapa Ulimwenguni Kama Kijana ambaye unaenda na Mafundisho ya Dini na Misingi yake MAMA hana siku Maalum Duniani ila siku zote ni zake kwa Taabu na Shida walizo zipata juu yetu Tusome kwa Pamoja katika Qur an ndani ya Surat Al- Isra Aya ya 23 M/Mungu anasema
"Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa heshma.
Na anaendelea kusema katika Aya inayofuata ya 24
Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni.
Abdallah Bin Masoud Amesema: Nilimuuliza Mjumbe Wa Mwenyezi Mungu; Ni amali ipi itanikaribisha niweze kuingia peponi? Mtume (S.A.W) akasema: Swala Kwa wakati wake, niakuliza tena na lipi jengine ewe Mjumbe Wa Allah? Akasema Mtume: Kuwafanyia wema wazazi wawili, nikauliza tena; na lipi jengine ewe Mjumbe Wa Allah? Mtume SAW Akasema; Kupigana jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
Kwa Maelezo haya Ewe Kijana Mwenzangu Tujitahidi kuwa karibu na wazazi wetu kila wakati kila Siku na sio Siku Maalum na Moja kwa Mwaka Hii Ndio Misingi ya Dini yetu na Mafundisho ya Dini yetu NAKUPENDA MAMA YANGU MPENDWA NA MAMA WA MARAFIKI ZANGU WOTE DAIMA
No comments:
Post a Comment