Monday, June 04, 2012

VITU AMBAVYO TUNAVITUMIA KWA KUJITWAHARISHIA


Ewe Ndugu yangu katika Imani katika Ukumbusho uliopita tulisimamia katika vitu vinne ambavyo kwa vitu hivyo tunajitwarisha navyo( Jisafisha) leo kwa Uwezo wa M/Mungu tutasimama kwa muda ili kupata vieleza Vitu hivyo.

1.MAJI.
Maji yanayofaa kutumika katika twahara kwa mtazamo wa fiqh hujulikana kama MAJI MUTLAQ ambayo haya yana sifa ya kuwa yenyewe ni twahara na yanaweza kutwaharisha kitu kingine.

Maji haya yako ya Aina Saba nayo ni :-

1:MAJI YA MVUA – haya ni yale yateremkayo kutoka mawinguni. Mwenyezi Mungu anatuambia juu ya maji haya:.
"NA TUNAYATEREMSHA KUTOKA MAWINGUNI MAJI SAFI (kabisa) (25:48) Qur an Surat Al -Furqan
Na M/MUNGU anasema tena katika Sura nyengine
Na akasema tena:
"NA AKAKUTEREMSHIENI MAJI KUTOKA MAWINGUNI ILI KUKUTWAHIRISHENI(kukusafisheni ) KWAYO…"(8:11) Qur an Surat Anfal

2: MAJI YA THELUJI
Haya ni yale yateremkayo kutoka mawinguni yakiwa katika hali ya kumiminika kisha ya kaganda.

3: MAJI YA UMANDE
Haya ni yale yateremkayo kutoka mawinguni yakiwa katika hali ya kuganda kisha yaka yeyuka yanapofika ardhini.
Mtume anatuambia katika kuonyesha utwahara wa aina hizi za maji:
"Ewe Mola wa haki nikoshe kutokana na makosa yangu kwa theluji, maji na (maji ya) umande"

4:MAJI YA BAHARI
Yaani tunamaanisha maji ya chumvi.

5:MAJI YA MAZIWA NA MITO
Yaani tunamaanisha maji matamu yasiyo na chumvi.
Imepokelewa na Abu- Hurayrah- Allah amridhie amesema: Mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu – Allah amrehemu na kumshushia amani – akasema:Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu sisi tunasafiri, na tunachukua maji kidogo tu, tukiyatumia kutawadhia tutashikwa na kiu, je, tutawadhe kwa maji ya bahari? Mtume akamjibu:"Hiyo (bahari) ni twahara maji yake na halali mfu(maiti) wake " Mutafaq 3laih.

6:MAJI YA CHEMCHEM
Haya ni yale yachimbukayo yenyewe kutoka ndani ya ardhi bila ya kutumia zana kuyatoa.

7:MAJI YAVISIMA
Hayo ni yale yachimbuliwayo kutoka ardhini.
Aina zote hizi za maji tulizozitaja na ambazo zinazofanana na hizi inafaa kuyatumia katika twahara yakiwa peke yake au yakichanganywa pamoja baina aina moja na nyingine.

Inshallah Ewe Kijana Mwenzangu Zingatia haya Machache Inshallah tutakuja Kumalizia Aina zilizobaki katika Vitu ambavyo tunaweza kujitwaharisha kutokana na vitu hivyo.
Ndugu yenu katika Imani katika Uislam Tuombeane Dua Njema Na tujenge tabia ya kutakiana mema na mazuri KWA PAMOJA DAIMA TUNAWEZA.

No comments:

Post a Comment