Monday, June 04, 2012

TWAHARA


Ewe kijana mwenzangu Inshallah kwa uwezo wake Mungu tunaendelea 
Ukumbusho katika Mlango Twahara.
Baada ya kuona aina za Maji ambazo inafaa kwa Mtu kujitwaharisha(Kujisafisha) tuliendelee kuangalia Vitu Vyengine ambavyo inafaa kuvitumia kwa ajili ya kujitwaharishia (kujisafisha)

2.MCHANGA
Mchanga hutumika katika twahara badala ya maji ikiwa mtu amekosa maji au maji yapo lakini hawezi kuyatumia kwa sababu ya maradhi ambayo akitumia maji yatazidi au yatachelewa kupona.Twahara hii ya kutumia mchanga badala ya maji ndio hujulikana katika sheria kama TAYAMMAMU. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:- "NA KAMA MKIWA WAGONJWA (mmekatazwa kutumia maji) AU MMO SAFARINI AU MMOJA WENU AMETOKA MSALANI (chooni) AU MMEWAGUSA WANAWAKE NA MSIPATE MAJI BASI UKUSUDIENI (tayamamuni) UDONGO SAFI, MPAKE NYUSO ZENU NA MIKONO YENU…" (4:43)

3.DAB-GH
Hii ni njia/utaratibu utumikao katika kuitwaharisha ngozi ya mnyama ili iweze kufaa kutumika katika matumizi mbalimbali ya binadamu. Hutumika vitu vikali kabisa vyenye muonjo wa tindikali kuondoa taka zilizo juu ya ngozi kama vile damu, mafuta na vipande vya nyama vilivyosalia wakati wa kuchuna. Baada ya hatua zote hizi ndipo ngozi hutiwa maji ikawa ni twahara inayoweza kutumiwa.

4.MAWE
Mawe au chochote chenye kufanana na mawe kama vile karatasi ( Toilet paper), na vinginevyo vinavyoweza kuondosha najisi hutumika katika kuchamba (kustanji) wakati yanapokosekana maji.(Ni bora zaidi kutumika Maji yanapo kuwepo)

Aina hizi za vitu vitumikavyo katika twahara zinaonyesha wepesi wa dini hii ya kiislamu katika kuweka sharia na hukumu zake ambazo zinakwenda sambamba na tabia na mazingira ya mwanadamu.
Haya yanathibitishwa na ruhusa tuliyopewa na sharia ya kujitwaharisha kwa kutumia aina zote za maji tulizozitaja na tukiyakosa maji au yakiwa yana tudhuru tumeruhusiwa kutumia mchanga.
Ukumbusho ujao Inshallah Tutaangalia Mgawanyo wa Maji na Hukumu zake Nataraji kutoka Kwenu Ushauri Maoni Mawazo na Kila Jema ambalo walifikiria katika kuliongezea Niwaombe Tena kwa Wale watakao pewa Uwezo wa Ku - comment kama utakuwa Na Swali nje ya Maudhui Tunakukaribisha katika GROUP MAMA LA KIJANA WA KIISLAM TANZANIA.
Inshallah Tushirikiane katika Kheri na tuwe wamoja Daima kwa Pamoja Tunaweza.
Mungu Tusaidie kwako twataraji kila zito kuwa Jepesi Amiin Amiin.

No comments:

Post a Comment