Tuesday, July 30, 2013

MAANA YA FUNGA

Neno Swaumu ambalo ni funga kilugha (Maana yake katika Lugha) ni Kujizuia

Ukijizuia na kula wewe unakuwa Umefunga.
Ukijizuia na Kuzungumza wewe unakuwa umefunga katika Maana ya Kilugha.

Dalili : Qur an

M/Mungu anasema katika kusimulia Kisa cha Bi Maryam "...Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu."Qur an Surat Maryam aya ya 26.

MAANA YA FUNGA KISHARIA .

Kujizuia/kujizuilia na vyenye kufuturisha [kufunguza] kuanzia kudhihiri alfajiri [ya pili] mpaka kuchwa [kuzama] kwa Jua pamoja na Nia.

Hii ndio Maana ya Funga.


Baadhi ya Wanawazuoni wameigawa Swaumu katika Vigawanyo Vikuu Viwili.

1.WAAJIB
2.SUNNA

Funga za Wajib ni kama Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambayo ni Nguzo katika Nguzo za Uislam.

Funga ya Kaffara na Nadhiri .

Funga za Sunna Mfano wa Funga za Jumatatu , Alhamis na Nyingi nyenginezo.

Angalizo :

Wapo wanachuoni wengine wamezigawa/wamezifanya Aina za Funga zaidi ya hizo Mbili kwa kuongeza Funga za Karaha , na Funga za Haraam .
  

HISTORIA YA FUNGA

Ndugu zangu wapendwa Tukumbuke kuwa Funga si ibada Ngeni, bali ni Ibada iliyofaradhishwa/Wajibishwa kwa WATU waliotangulia kabla yetu na pia kufaradhishwa katika umati huu wetu wa Mtume Muhammad Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani (S.AW).

Dalili

M/Mungu Subhanahu Wataallah anasema katika Qur an " Enyi mlioamini! mmelazimishwa kufunga [Swaumu] kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu". Qur an Suratul Baqarah aya ya 183.

Ama katika umati huu wa Mtume Muhammad Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani (S.AW) Funga ilifaradhishwa katika Mwezi wa Shaabani mwaka wa pili baada ya hijrah Mtume Muhammad (S.A.W).

Mtume (S.A.W) amefunga Miaka 9 na Baada ya hapo akafariki Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani.

Tumesema kuwa Funga ya Mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani ni Wajib na Ni Nguzo katika Nguzo za Uislam kwa Dalili zipi tunatolea Dalili kwa haya tunayo yasema InshaAllah Ukumbusho Ujao tutazieleza Dalili ambazo zimeifanya Funga ya Mwezi wa Ramadhani kuwa ni wa Wajib kutoka Qur an , Sunna na Ijmai za Wanawachuoni.
 


M/Mungu Subhanahu WataAla anasema katika Qur an

“ Enyi mlioamini mmelazimishwa kufunga (Saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha mungu. Qur an Suratul Baqarah aya ya 183.
Siku chache tu ( kufunga huko)...(Mwezi huo mlioambiwa mfunge) ….. “. Qur an Suratul Baqarah aya ya 184.

Ni mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa katika mwezi huo hii Qur-aani ili iwe uwongozi kwa watu, na hoja zilizo wazi wa uongozi na upambanuzi (wa baina ya haki na batili) Atakae Uona ( kuwa katika mji katika huu mwezi) (wa Ramadhani) afunge .…” Qur an Suratul Baqarah aya ya 185.

Dalili ya Hdithi

Imepokelewa hadithi kutoka kwa Abdullah ibn Umar M/Mungu amuwie Radhi amesema : Nimemsikia Mtume Muhammad (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani akisema: “ Umejengwa Uislam juu ya nguzo tano;

1.kushuhudia ya kwamba hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah Subhaanahu wa Ta3ala na hakika ya Mtume Muhammad (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie juu yake na Amani ni mtume wa M/Mungu.

2.Kudumisha Swala.

3.Kutoa Zakkah.

4.Kuhiji Katika Nyumba Tukufu Alkaaba Makkah (kwa Mwenye uwezo).

5.Kufunga Ramadhani ( Ushahidi wetu ) Kama alivyosema Mtume hadithi imepokewa na Imamu Bukhari na Muslim.

Na kuna hadithi nyingine nyingi zinazojulisha Uwajibu wa Funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Dalili katika Ijmai (Makubalino ya Wanawazuoni) kwa Mujibu wa Wanawazuoni wote wamekubaliana na kuwafikiana kwamba Funga ya Mwezi wa Ramadhani ni Wajib kwa Maana ni lazima kwa kila Muislam.

Ndugu yangu Muislamu

Hizi ndio Dalili ambazo zimeifanya Ibada ya Funga ya Mwezi wa Ramadhani kuwa Ni wajibu kwetu.


InshaAllah tuta endelea kuelezea  hukmu ya funga ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani 

Wabillahi - Taufiqh 

By :- Ghalib Nassor Monero l Azhary   

No comments:

Post a Comment