1.Kula au kunywa kwa kukusudia.
2.Kila kinachoingia tumboni au kooni kwa kukusudia.
3.Kukutana kimwili (kuingiliana) kati ya mume na mke.
4.Kujitoa Manii au kusababisha kutokwa na Manii (kwa kujichezea sehemu za siri, kukumbatiana au kupigana mabusu n.k
5. Kujitapisha kwa makusudi.
Imepokelewa hadith kutoka kwa Abu Hurayrah Radhi za M/Mungu zimshukie juu yake na Amani Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie juu yake na amani amesema " ...na mwenye kujitapisha basi inamuwajibikia kulipa". kama alivyosema Mtume (Wameipokea Maimamu watano).
6.Kutokwa na Damu ya Mwezi (Hedhi) au Damu ya Uzazi ( nifasi ).
Na tukasema kwamba hukmu za Mambo haya zimegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo tuliahidi kwa uwezo wa M/Mungu katika Post hii tutayaeleza hukmu hizo.
Ndugu yangu Mpendwa katika Imani Fahamu kwamba Mambo haya tuliyo yaeleza yenye kuharibu funga kwa upande wa HUKMU ZAKE pale yanapo mtokea Mtu yapo ambayo yanampasa Mtu
1.KULIPA.
2.KULIPA NA KAFARA .
Mambo yote tuliyoyataja ukitoa namba tatu (3) yanabeba/yanachukua Hukmu ya Namba Moja Namba Tatu lina Chukua Hukmu ya Namba 2.
KAFARA
tuliposema katika hukmu ya Mtu mwenye kumuingilia Mke wake Mchana wa wa Mwezi wa Ramadhani alipe na kafara tunamanisha kulipa hapo ni kulipa ile siku ambayo ameiharibu funga yake kwa kumuingilia Mke wake baada ya Ramadhani.
Ama kafara iko katika Mpangilio kama ufuuatao :-
1.Kumuachia Huru Mtumwa - Alhamdullilah utumwa hakuna siku hizi.
2.Kufunga Miezi Miwili mfululizo ikiwa hawezi
3.Kulishiza/lisha Maskini 60
na vile vile inampasa kuleta Istighfaari kwa Mola wale kwa kosa alilo litenda kwa kuingilia Mchana wa Mwezi Ramadhani M/Mungu ndiye Mjuzi zaidi
BY : GHALIB NASSOR MONERO L AZHARIY
No comments:
Post a Comment