Tuesday, July 30, 2013

NGUZO YA IHSANI

NGUZO YA TATU NA YA MWISHO NI YA  IHSANI.

Na Nguzo yake ni Moja nayo ni:-

1.Kumuabudu Allah kama unamuona Kama humuoni yeye anakuona wewe.

Huu kwa muhtasari ndio Uislamu, dini na mfumo sahihi na kamili wa maisha kwa wanadamu wote waliochaguliwa na Allah Mola Muumba wao:

Rejea Dalili ya Aya Qur an 

"… LEO NIMEKUKAMILISHENI DINI YENU NA KUKUTIMIZIENI NEEMA YANGU NA NIMEKUPENDELEENI UISLAMU UWE DINI YENU...” (5:3) 

tuelewa na tufahamu kwamba kuishi nje ya dini hii ni kulikana umbile lako kwani UISLAMU NI HAKI YAKO YA KUZALIWA uliyopewa hadiya (zawadi) na Mola Muumba wako.

"Kila chenye kuzaliwa huzaliwa katika UISLAM ..." Kama alivyosema Mtume .

Angalizo 

Ewe Kijana wa Kiislam mpaka hapa  tutakuwa tumefahamu kwa Muhtasari (ufupi).

1.NGUZO ZA UISLAMU
2.NGUZO ZA IMANIE.
3.NGUZO YA IHSAN

Tunawatakia Funga Njema na yenye baraka na M/Mungu atujaalie wenye kuudiriki Usiku wa Laylatul Qadir (Usiku wa cheo ) katika Ibada .

No comments:

Post a Comment