Baadhi ya Dua za Qur'ani Tukufu .
baadhi ya Dua za Qur an tukufu.
baadhi ya Dua za Qur an tukufu.
رَبَّنَا آتِنَا فِي الدُّنْيَا حَسَنَةً وَفِي الآخِرَةِ حَسَنَةً وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ
1. Mola wetu Mlezi, tupe duniani mema, na Akhera mema, na utulinde na adhabu ya Moto! Qur an 2:201.
رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ
2. Mola wetu Mlezi! Tumiminie subira, na isimamishe imara miguu yetu, na utusaidie tuwashinde watu Makafiri Qur an 2:250.
رَبَّنَا لاَ تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا
3. Mola wetu Mlezi! Usituchukulie tukisahau au tukikosea. Qur an 2:286.
رَبَّنَا وَلاَ تَحْمِلْ عَلَيْنَا إِصْرًا كَمَا حَمَلْتَهُ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِنَا
4. Mola wetu Mlezi! Usitubebeshe mzigo kama ulio wabebesha wale walio kuwa kabla yetu. Qur an 2:286.
رَبَّنَا وَلاَ تُحَمِّلْنَا مَا لاَ طَاقَةَ
لَنَا بِهِ وَاعْفُ عَنَّا وَاغْفِرْ لَنَا وَارْحَمْنَا أَنتَ مَوْلانَا
فَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ
5. Mola wetu Mlezi Usitutwike tusiyo
yaweza, na utusamehe, na utughufirie, na uturehemu. Wewe ndiye Mlinzi
wetu. Basi tupe ushindi tuwashinde kaumu ya makafiri. Qur an 2:286.
رَبَّنَا لاَ تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ
6. Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo
zetu baada ya kwisha tuongoa, na utupe rehema itokayo kwako. Hakika Wewe
Ndiye Mpaji. Qur an 3:8.
رَبَّنَا إِنَّكَ جَامِعُ النَّاسِ لِيَوْمٍ لاَّ رَيْبَ فِيهِ إِنَّ اللَّهَ لاَ يُخْلِفُ الْمِيعَادَ
7. Mola wetu Mlezi! Tughufirie madhambi
yetu na kupita kwetu kiasi katika mambo yetu, na isimamishe imara miguu
yetu na utunusuru tuwashinde kaumu ya makafiri. Qur an 3:147.
رَبَّنَا إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ النَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَار
8. Mola wetu Mlezi! Hakika unaye mtia Motoni umemhizi; na walio dhulumu hawana wasaidizi. Qur an 3:192.
رَّبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًا يُنَادِي لِلإِيمَانِ أَنْ آمِنُواْ بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا
9. Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tumemsikia
mwenye kuita akiitia Imani kwamba: Muaminini Mola wenu Mlezi; nasi
tukaamini. Qur an 3:193.
رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الأَبْرَارِ
10. Mola wetu Mlezi! basi tusamehe madhambi yetu, na utufutie makosa yetu, na utufishe pamoja na watu wema. Qur an 3:193.
رَبَّنَا وَآتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَى رُسُلِكَ وَلاَ تُخْزِنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّكَ لاَ تُخْلِفُ الْمِيعَادَ
11. Mola wetu Mlezi! Na utupe uliyo tuahidi kwa Mitume wako, wala usituhizi Siku ya Kiyama. Hakika Wewe huvunji miadi. Qur an 3:194.
رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ
12. Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi
zetu, na kama hutusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye
kukhasirika.Qur an 7:23.
رَبَّنَا لاَ تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
13. Mola Mlezi wetu! Usitujaalie kuwa pamoja na watu walio dhulumu. Qur an 7:47.
رَبَّنَا افْتَحْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمِنَا بِالْحَقِّ وَأَنتَ خَيْرُ الْفَاتِحِينَ
14. Ewe Mola Mlezi wetu! Tuhukumie baina yetu na kaumu yetu kwa haki, nawe ndiye mbora wa wanao hukumu. Qur an 7:89.
رَبَّنَا أَفْرِغْ عَلَيْنَا صَبْرًا وَتَوَفَّنَا مُسْلِمِينَ
15. Ewe Mola Mlezi wetu! Tumiminie uvumilivu na utufishe hali ni Waislamu. Qur an 7:126.
رَبَّنَا لاَ تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ. وَنَجِّنَا بِرَحْمَتِكَ مِنَ الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ
16. Ewe Mola wetu Mlezi! Usitufanye wenye
kutiwa misukosuko na hao watu madhaalimu. Na utuokoe kwa rehema yako na
watu makafiri. Qur an 10:85-86.
رَبَّنَا إِنَّكَ تَعْلَمُ مَا نُخْفِي وَمَا نُعْلِنُ وَمَا يَخْفَى عَلَى اللَّهِ مِن شَيْءٍ فِي الأَرْضِ وَلاَ فِي السَّمَاء
17. Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe unajua
tunayo yaficha na tunayo yatangaza. Na hapana kitu kinacho fichikana
kwa Mwenyezi Mungu katika ardhi wala katika mbingu. Qur an 14:38.
رَبَّنَا آتِنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًا
18. Mola wetu Mlezi! Tupe rehema itokayo kwako, na tutengezee uwongofu katika jambo letu. Qur an 18:10.
رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا
19. Mola wetu Mlezi! Tupe katika wake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wachamngu. Qur an 25:74.
رَبَّنَا وَسِعْتَ كُلَّ شَيْءٍ رَّحْمَةً
وَعِلْمًا فَاغْفِرْ لِلَّذِينَ تَابُوا وَاتَّبَعُوا سَبِيلَكَ وَقِهِمْ
عَذَابَ الْجَحِيمِ
20. Mola wetu Mlezi! Umekienea kila kitu
kwa rehema na ujuzi. Basi wasamehe walio tubu na wakaifuata Njia yako,
na waepushe na adhabu ya Jahannamu.Qur an 40:7.
رَبَّنَا وَأَدْخِلْهُمْ جَنَّاتِ عَدْنٍ
الَّتِي وَعَدتَّهُم وَمَن صَلَحَ مِنْ آبَائِهِمْ وَأَزْوَاجِهِمْ
وَذُرِّيَّاتِهِمْ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ
21. Mola wetu Mlezi! Na waingize katika
Bustani za Milele ulizo waahidi. Na uwape haya pia wale walio fanya mema
miongoni mwa wazee wao na wake zao na dhuriya zao. Hakika Wewe ni
Mwenye nguvu, Mwenye hikima. Qur an 40:8.
رَبَّنَا اكْشِفْ عَنَّا الْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ
22. Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini. Qur an 44:12.
رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا
الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالإِيمَانِ وَلا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا
لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَؤُوفٌ رَّحِيمٌ
23. Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na
ndugu zetu walio tutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo
zetu undani kwa walio amini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na
Mwenye kurehemu. Qur an 59:10.
رَّبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ
24. Mola wetu Mlezi! Juu yako tumetegemea, na kwako tumeelekea, na kwako ndio marejeo. Qur an 60:4.
رَبَّنَا أَتْمِمْ لَنَا نُورَنَا وَاغْفِرْ لَنَا إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
25. Mola wetu Mlezi! Tutimilizie nuru yetu, na utughufirie! Hakika Wewe ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. Qur an 66:8.
No comments:
Post a Comment