Wednesday, August 14, 2013

MALIPO YA KILA KITENDO CHA MJA HULIPWA KWA MUJIBU WA NIA YAKE

                           " إنما الأعمال بالنيات "

MALIPO YA KILA KITENDO CHA MJA HULIPWA KWA MUJIBU WA  NIA YAKE.
Kutoka kwa Kiongozi  wa Waumini, Abu Hafs 'Umar Ibn Al Khattaab Radhi za Allah zimshukie Juu yake na Amani ambaye alisema : Nilimsikia Mjumbe wa Mwenyeezi  Mungu (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani akisema:
Vitendo vinategemea (vinalipwa kwa) nia na kila mtu atapata kwa mujibu wa kile alichokusudia.  Kwa hivyo yule aliyehama  kwa ajili ya Allaah na Mtume wake, uhamaji wake ni kwa ajili ya Allaah na Mtume wake, na  yule ambae uhamaji wake ulikuwa ni kwa ajili ya manufaa ya kidunia au kwa ajili ya kumuoa mwanamke (Fulani)  uhamaji wake ulikuwa kwa kile kilichomuhamisha.
Imesimuliwa na Maimam wawili mabingwa wa hadithi Abu Abdalla Muhammad  Ibn Ismail Ibn Ibrahim Ibn Mughiyra Ibn Bardizbah Al Bukhari na Abu Al Husayn Muslim Ibn Al-Hajjaj Ibn Muslim Al Qushayri An-Naysaburi, katika sahihi zao mbili ambavyo ni vitabu vya kutegemewa. 
 -----------------------------------------------------------------------------
  عن أَمِيرِ المُؤمِنِينَ أَبي حَفْصٍ عُمَرَ بنِ الخطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ : سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ:   ((إِنَّما الأَعْمَالُ بالنِّيَّاتِ وإنَّما لكُلِّ امْرِىءٍ ما نَوَى، فَمَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ فَهِجْرَتُهُ إلى اللهِ ورَسُولِهِ، ومَنْ كانَتْ هِجْرَتُهُ لِدُنْيا يُصِيبُها أو امْرأةٍ يَنْكِحُها فَهِجْرَتُهُ إلى ما هَاجَرَ إليه)).  
رَوَاهُ إِمَامَا الْمُحَدِّثِينَ أَبُو عَبْدِ اللهِ مُحَمَّدُ بنُ إِسْمَاعِيل بن إِبْرَاهِيم بن الْمُغِيرَة بن بَرْدِزبَه الْبُخَارِيُّ     وَأَبُو الْحُسَيْنِ مُسْلِمٌ بنُ الْحَجَّاج بن مُسْلِم الْقُشَيْرِيُّ النَّيْسَابُورِيُّ   رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا فِي "صَحِيحَيْهِمَا" اللذينِ هُمَا أَصَحُّ الْكُتُبِ الْمُصَنَّفَةِ.

No comments:

Post a Comment