KUJA KWA JIBRIIL KUWAFUNDISHA WAISLAMU MAMBO YA DINI YAO
Imesimuliwa na Muslim.
-----------------------------------------------------------
Kutoka kwa 'Umar Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake amesema: Siku moja tulikuwa tumekaa na Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani,
Mara alitokea mtu katika hiko kikazi ambacho tulichokaa ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe sana na nywele
zake zilikuwa nyeusi sana; hakuwa na alama ya machovu ya safari na wala
hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu
na Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani, akaweka
magoti yake karibu na magoti yake (Mtume) (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani, na akaweka viganja vyake juu
ya mapaja yake kisha akasema; Ewe Muhammad! Niambie kuhusu Uislamu.
Mjumbe wa Allaah alisema:
Uislamu ni kukiri kuwa hakuna mola isipokuwa Allaah na Muhammad ni
Mjumbe wake, kusimamisha Swalah, kutoa Zakaah, kufunga Ramadhaan na
kwenda kuhiji (Makkah) ukiweza.
(Akasema
yule mtu yaani Jibriyl) Umesema kweli. Tulipigwa na mshangao kwa
kumuuliza kwake Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani, na kumsadikisha. Na akasema tena: Niambie kuhusu
Imani. akasema Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani Ni
kumuamini Mwenyeezi-Mungu, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake na
siku ya Qiyaama, na kuamini ya kuwa kheri na shari zinatoka Kwake M/Mungu Mtukufu .
Akasema Jibriyl: Umesema kweli, akasema hebu nielezee kuhusu Ihsani. Akasema Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani, Ni kumuabudu M/mungu Mtukufu kama vile unamuona na kama humuoni basi Yeye Anakuona. Akasema (Jibriyl): Niambie kuhusu Qiyaama. Akajibu Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani, Muulizwaji si mjuzi kama vile Muulizaji (kwa Maana kwamba wewe Jibriyl ndiye Mjuzi zaidi kuhusu Qiyaama) . Kisha akamwambia: Nijulishe alama zake: Akajibu Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani, Kijakazi atazaa bibi yake, na utaona wachunga wenda miguu chini, wenda
uchi (wasio na uwezo wa kumiliki hata mavazi), mafukara (wasiokuwa hata
na sehemu ya kuishi kwa umaskini) wakishindana kujenga majumba ya
fahari. Kisha akaondoka (Jibriyl) na nilitulia kidogo (nikitafakari).
Kisha akasema Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani, "Ewe 'Umar! Je, unamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza? Nikasema: Allaah na Mjumbe wake wanajua zaidi. Akasema Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani, Ni Jibriyl, alikuja kuwafundisha dini yenu.
-----------------------------------------------------------
"مجىء جبريل ليعلم المسلمين أمر دينهم"
عَن
عُمَر رضي اللهُ عنه أَيْضاً قال: بَيْنَما نَحْنُ جُلْوسٌ عِنْدَ
رسُولِ الله صلى الله عليه وسلم ذات يَوْم إذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ
شَدِيدُ بَياضِ الثِّيَاِبِ شَديدُ سَوَادِ الشَّعْرِ، لا يُرَى عليه
أَثَرُ السَّفَرِ ولا يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ، حَتى جَلَسَ إلى النَّبِّي
صلى الله عليه وسلم، فأسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إلى رُكْبَتَيْهِ ووَضَعَ
كَفَّيْهِ على فَخِذَيْهِ، وقال: يا محمَّدُ أَخْبرني عَن الإسلامِ، فقالَ
رسُولُ الله صلى الله عليه وسلم:(( الإسلامُ أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لا إلهَ
إلا اللهُ وأَنَّ محمِّداً رسولُ الله، وتُقِيمَ الصَّلاةَ، وتُؤتيَ
الزَّكاةَ، وتَصُومَ رَمَضان، وتَحُجَّ الْبَيْتَ إن اسْتَطَعتَ إليه
سَبيلاً)). قالَ صَدَقْتَ. فَعَجِبْنا لهُ يَسْأَلُهُ ويُصَدِّقُهُ، قال :
فَأَخْبرني عن الإِيمان. قال: ((أَن تُؤمِنَ باللهِ، وملائِكَتِهِ
وكُتُبِهِ، ورسُلِهِ، واليَوْمِ الآخِرِ، وتُؤمِنَ بالْقَدَرِ خَيْرِهِ
وشَرِّهِ)) قال صدقت. قال : فأخْبرني عَنِ الإحْسانِ. قال:(( أنْ تَعْبُدَ
الله كَأَنَّكَ تَرَاهُ فإنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فإنَّهُ يَرَاك)). قال:
فأَخبرني عَنِ السَّاعةِ، قال: ((ما المَسْؤولُ عنها بأَعْلَمَ مِنَ
السَّائِلِ )). قال: فأخبرني عَنْ أَمَارَتِها، قال:(( أن تَلِدَ الأمَةُ
رَبَّتَها، وأَنْ تَرَى الحُفاةَ العَُراةَ العالَةَ رِعاءَ الشَّاءِ
يَتَطَاوَلُونَ في الْبُنْيانِ )) ثُمَّ انْطَلَقَ، فَلَبِثْتُ مَلِيّاً،
ثُمَّ قال : ((يا عُمَرُ، أَتَدْرِي مَنِ السَّائِلُ؟)) قُلْتُ: اللهُ
ورسُولُهُ أَعلَمُ . قال:(( فإِنَّهُ جِبْرِيلُ أَتاكُمْ يُعَلِّمُكُمْ
دِينَكُمْ))
رَوَاهُ مُسْلِمٌ
No comments:
Post a Comment