Friday, August 30, 2013

RAIS WA ZANZIBAR AKUTANA NA WATANZANIA WANAOISHI NCHINI UHOLANZI.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Holland..Rais Shein yupo nchini Holland kwa ziara ya kikazi. 
Balozi wa Tanzania nchini Belgium Mh: Diodorus Kamala akifungua mkutano uliojumuisha Watanzania wanaoishi nchini Holland kuzungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr Ali Mohamed Shein hapo jana katika hotel ya Hilton iliyopo jijini Den Haag. 
 Mwenyekiti wa Tane nchini Uholanzi ndugu Kweba Bulemo akimkabidhi zawadi ya kitabu maalumu Mheshimiwa Rais Dr.Ali Mohamed Shein kama kumbukumbu alipofanya mazungumzo na Watanzania hao hapo jana nchini Uholanzi.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akitoa ufafanuzi wa maswali yote aliyokuwa akiulizwa na baadhi ya Watanzania kuhusu mustakabari wa Kisiwani Zanzibar
 Pichani ni mahudhurio ya watanzania waliojitokeza kuzungumza na Mh:Rais Ali Mohamed Shein hapo jana katika ukumbi wa hotel ya Hilton
 Kati ya Watanzania waliouliza maswali ndugu Omary Abbas alikuwa mmoja wapo..pichani akiuliza moja kati ya maswali yake hapo jana.
 Baadhi ya Watanzania wakiwa makini kabisa kusikiliza nini Rais anazungumza.
 Wake kwa waume walijitokeza kwa wingi katika mkutano huo na Mheshimiwa Rais wakiwa makini kusikiliza 
 Maganga One Blogger akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi hapo jana.
Maganga One Blogger akiwa na Mheshimiwa Balozi Diodorus Kamala hapo jana katika mkutano wa wa Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Uholanzi[Picha zote na maelezo toka http://magangaone.blogspot.com/ .. Kwa picha zaidi bonyeza habari zaidi/read more




No comments:

Post a Comment