Kwa mujibu wa mashtaka aliyosomewa akiwa MOI, Sheikh Ponda atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapotajwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Wakili Nassor Jumaa anayesimamia Katibu
wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (54)
ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi mpya ya kufanya uchochezi katika
maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezungumzia
kitendo cha kumhamisha mteja wake kutoka hositalini hadi Segerea.
Leo hii majira ya saa 7 mchana nje ya viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam amesema kuwa amesikitishwa na hatua ya vyombo vya dola kumuondoa Sheikh Ponda aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Kitengo cha Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu na kisha kumhamishia katika gereza la Segerea.
Wakili Jumaa amesema amesikitisha na kitendo hicho kwani muda mfupi baada ya wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kumaliza kumsomea Sheikh Ponda shitaka linalomkabili, Hakimu Hellen Riwa alitoa amri ya kukaa chini ya ulinzi Sheikh Ponda aendelee na matibabu.
Jumaa akaongeza kuwa ameshangazwa kuona leo, wanausalama wamemtoa Sheikh Ponda wodini na kumpeleka katika gereza la Segerea na kwamba atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapojatwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
“Kwa kweli kitendo hicho kime nisikitisha na kunishitua sana… ila tunatafakari ni hatua gani za kisheria tutazichukua huko siku za usoni,”alisema Jumaa.
Kwa upande wao familia ya Sheikh Ponda wamesema wanalaani kitendo
kilichofanywa na serikali cha kumuondoa ndugu yao hospitalini huku akiwa
anaendelea kupata matibabu.Msemaji wa familia hiyo Is-haq Rashid,
alisema kutokana na hali hiyo kama familia wanalirudisha suala la Sheikh
Ponda kwa uongozi wa jumuiya na Taasisi za kiislamu kwa ajili ya hatua
zaidi ya kuhakikisha kiongozi mwenzao anakuwa salama.“Uporaji huu wa
mgonjwa unazidi kutupa mashaka juu ya dhamira ya serikali hasa ikiwa
tunalituhumu jeshi la polisi katika kumdhuru Sheikh,hatujui kwanini kila
wakati wanafanya mambo yao kwa kuvizia kama mwanzoni
tuliwaomba viongozi wenzie wawe na subira juu ya yaliyotokea sasa
tunaachia hili walizungumzie wao.”alisema Is-haq.Leo hii majira ya saa 7 mchana nje ya viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam amesema kuwa amesikitishwa na hatua ya vyombo vya dola kumuondoa Sheikh Ponda aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Kitengo cha Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu na kisha kumhamishia katika gereza la Segerea.
Wakili Jumaa amesema amesikitisha na kitendo hicho kwani muda mfupi baada ya wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kumaliza kumsomea Sheikh Ponda shitaka linalomkabili, Hakimu Hellen Riwa alitoa amri ya kukaa chini ya ulinzi Sheikh Ponda aendelee na matibabu.
Jumaa akaongeza kuwa ameshangazwa kuona leo, wanausalama wamemtoa Sheikh Ponda wodini na kumpeleka katika gereza la Segerea na kwamba atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapojatwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
“Kwa kweli kitendo hicho kime nisikitisha na kunishitua sana… ila tunatafakari ni hatua gani za kisheria tutazichukua huko siku za usoni,”alisema Jumaa.
![]() |
Hati ya mashtaka aliyoshitakiwa Sheikh Ponda Issa Ponda. |
No comments:
Post a Comment