Thursday, August 15, 2013

Siku moja baada ya ziara ya kushtukiza ya waziri wa uchukuzi Dk. Harison Mwakyembe, kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar-es-Salaam, kiasi kikubwa cha dawa za kulevya kimekamatwa uwanjani hapo katika harakati za kusafirishwa kwenda nchi za nje.
Dawa hizo aina ya Heroni kete 86 na bangi misokokoto 34 iliyokuwa ikisafirishwa na mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Lenard Jeremia Monyo,akiwa katika harakati za kuzisafirisha kwenda Italia kupitia Zurich Uswis kwa shirika la ndege la Swiss Air, waziri Mwakyembe amesema wafanyakazi wa mamlaka ya viwanja vya ndege na jeshi la polisi kiwanjani hapo walimbaini mtuhumiwa huyo na kuahidi kufuatilia kesi hiyo mpaka mwisho wake kwani haina haja ya upelelezi kwani kila kitu kipo wazi.

Kuhusu kutaja majina na picha za watuhumiwa wa usafirishaji wa dawa za kulevya kwenda nje ya nchi,waziri Mwakyembe amesema kuwa, anasubiri kupata ushaidi na vielelezo vya majina na picha,na kuwa kuanzia sasa wale wote watakao kamatwa na dawa za kulevya picha zao zitachapishwa na kutangazwa kwenye vyombo vya habari ikiwemo kilo 120 zilizokamatwa Afrika ya kusini.

Waziri Mwakyembe amewaagiza viongizi wa mamlaka ya viwanja vya ndege kuona namna ya kuwa zawadi vijana hao wa vyeo na kupandishwa mshahara jambo alilosema atalifuatilia kuona utekelezaji wake,huku akidai kuwa watakaofanywa vizuri watapongezwa na wale watakao haribu watafukuzwa kazi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,na kuwa wanaona utaratibu wa kuscan mizigo yote inayopitia uwanja wa ndege na bandarini.

Awali waziri Mwakyembe amesema kuwa hakuna mwenye uhakika na maisha yake kuwa ana mkataba na Mungu alipoulizwa juu ya usalama wake kufuatia mtandao huo kuwa mkubwa ambapo pengine unaweza kuhatarisha maisha yake,na kuwataka idara zote zinazo husika na uwanjani hapo kushirikina kwa pamoja katika kusafisha jina baya lililopata uwanja huo wenye kuwenzi jina la baba wa taifa la Tanzania hayati Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere.

CHANZO: ITV

No comments:

Post a Comment