Wednesday, August 21, 2013

SWAUTUN NAQY NA  ALBUM MPYA .  
Kikundi cha Swautun Naqiy chenye makazi yake Temeke Vetenari jijini Dar es salaam,kimefanya  uzinduzi wa Album ya Qaswida Mpya  inayojulikana kwa jina la AMANI YA TANZANIA. 
Album hiyo imezinduliwa siku ya Eid pili katika viwanja vya mnazi Mmoja ambapo mgeni rasmi alikuwa kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum Suleiman Kova.
 USTAADH MOHAMMAD MUHIYA KIONGOZI WA KIKUNDI CHA SWAUTINN NAQY AMBACHO KINAJIHUSISHA NA KUTOA UJUMBE MWEMA KWA NJIA YA QASWIDA.
katika uzinduzi huo kikundi cha Swautin Naqy kilitambulisha kaswida zake sita ambazo zinapatikana katika Album ya  Amani Tanzania Nazo ni Mke mwema,Saluqalbi,Wagonjwa,Pongezi kwa akina baba na Pongezi kwa akina mama kaswida ambayo ilitokea kutamba katika miaka ya nyuma.
Akijibu swali la mwandishi wa munirablog ambaye aliyepata Ongea na Ustaadh Mohammad Muhiya ambaye ni kiongozi wa Kikundi Muandishi alimuuliza  sababu ya kutunga Qaswida inayozungumzia Amani ya Tanzania,ustaadh muhiya alisema "Hii Amani tuliyopewa na ALLAH ni tunu kwenu,tukae tukitambua kwamba hatutakiwi kuichezea kwa namna yoyote,tunawajibika kuilinda kwa gharama yoyote,kwani ikituponyoka, kuipata tena itakuwa ngumu sana,sasa mimi ambaye nimejipa dhamana ya kufikisha ujumbe kwa njia hii ya tungo ya qaswida nikaona ni vyema nami nitoe mchango wangu juu ya Amani ya Tanzania.".mwisho wa kumnukuu.

Katika Uzinduzi wa Album hiyo kulikuwepo Vikundi mbalimbali kama vile  Firqatu salaam chini ya uongozi wa ustaadh Khamis Mshauri na madrasat Thanawiyyah ya Temeke.

No comments:

Post a Comment