TINDIKALI YAUZWA KWEUPE
LICHA ya serikali kutangaza kudhibiti upatikanaji holela wa tindikali, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa kimiminika hicho bado kinapatikana kirahisi mitaani.
Jumatatu iliyopita, mapaparazi wetu walizama mitaani na kuanza kuisaka bidhaa hiyo ili kuona kama upatikanaji wake una ugumu wowote.
Mapaparazi hawakuishia hapo, walifika hadi Kipawa jijini Dar ambapo walikutana na mwalimu mmoja wa shule ya sekondari ambaye alisema anaiuza bidhaa hiyo kwa shilingi 16,000 tu na hashushi zaidi ya hapo. Tindikali hiyo ni mali ya shule.
Ili kuithibitisha kuwa ni tindikali kweli, aliwapa mapaparazi makaratasi maalum (litmus paper) ambayo hutumiwa kufanyia ‘test’ kitaalam.
Makaratasi hayo hubadilika rangi toka bluu kuwa mekundu kila yanapokutana na tindikali na kuashiria kuwa ni yenyewe. Wakati akiendelea kuchanganya, mara kadhaa wanafunzi waliingia lakini aliwatoa nduki.
Hadi mapaparazi wetu wanaondoka shuleni hapo, mwalimu huyo hakujua kama wanunuzi waliokwenda kununua tindikali hiyo ni ‘wapelelezi’ mahiri kutoka Global Publishers.
Mpaka sasa, Watanzania wengi wameshamwagiwa tindikali na watu wanaosadikiwa ni wabaya wao. Miongoni mwa watu waliokumbwa na balaa hilo ni mmiliki wa Home Shopping Center, Said Mohamed Saad, Shehe wa Bakwata wilayani Arumeru, Issa Makamba na mtu aliyedaiwa ni mpiga debe wa CCM, Igunga Mussa Tesha.
Wengine ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo, Katibu wa Mufti Zanzibar, Shehe Fadhili Soraga na wasichana wawili raia wa Uingereza, Kirstie Trup na Katie Gee.
Pichani juu ni baadhi ya wananchi waliomwagiwa tindikali.
Habari na : Chande Abdallah na Hans Mloli
No comments:
Post a Comment