Friday, August 09, 2013

VIONGOZI WAISLAM KUWENI CHACHU YA MAENDELEO KWA WAISLAM.


Tanzania ni nchi yenye Dini na Itikadi tofauti , Moja katika Dini ambazo zipo Tanzania ni Dini ya Uislamu,Dini ambayo kwa Makadirio ya sensa zilizo hakikiwa kuwa ndio yenye watu wengi wanao ishi katika Nchi hii.

Serikali ya Tanzania  ni Serikali ambayo inaongozwa na Katiba isiyokuwa  Qur an na Sunna , katika Serikali hii  Viongozi na Watendaji  wamejiwekea Mipaka na kutengeneza kauli Mbiu kuwa Serikali ya Tanzania haina Dini.

hii ikiwa na Maana kwamba Serikali zina ongozwa na Katiba ambayo imetungwa na Vyombo Maalumu ambavyo vimeteuliwa.

Katika Serikali ya Tanzania Viongozi wengi wa Ngazi mbali mbali za Chini na Juu ni Waislamu , Tunamshukuru M/Mungu baadhi yao wamekuwa Mstari wa Mbele katika kushiriki Shughuli  za Kiimani  pale wanapo alikwa bila ya kipingamizi chochote .

hii inaonyesha kwamba ni watu ambao  wanajali , hongera zao  kwa hilo .

Tunawaombea kwa M/Mungu wakiwa kama Waislamu na si kama viongozi wa Serikali wa Ngazi yoyote  ili msitoke Nje ya Katiba. 

Jitoleeni kwa hali na Mali katika kuendeleza Waislamu wenzenu katika Nyanja Mbalimbali za Kimaaendeo na Kimaisha kwa Ujumla.

leo Taasisi nyingi  za Kiislamu ziko nyuma sana kulinganisha na za wasio kuwa waislamu kwa sababu nyingi sana .

Kwa Imani yenu Saidieni katika kuleta Maendeleo katika hizi Taasisi  kwani kufanya hivyo ni chachu ya Maendeleo kwa Taifa pia.

Vile vile nitoe wito kwa Viongozi wa Dini kuweni ni wenye kuwakumbusha Ndugu zenu viongozi katika Maendeleo ya Taasisi zetu na Jamii kwa Ujumla  na  si kuridhika na kuwaalika katika Makongamano yetu , Shughuli zetu za Maulid au kujitengenezea yako binafsi.

la pili kwa Viongozi wa Dini  tuwe watekelezaji  wa Mipango ya Kimaendeleo  kikweli katika Michango na Misaada tunayo ipata sio ingie katika Mifuko yetu na mambo yetu binafsi.

Mwisho kabisa Nijumuishe katika Neno Viongozi na waislamu wote wenye uwezo SAIDIA HARAKATI ZA WAISLAMU TANZANIA.

No comments:

Post a Comment