Watanzania
waishio nchi za nje wametakiwa kuwalea watoto wao katika misingi bora
ya malezi yanayofuata mila, desturi na utamaduni wa mtanzania ili
waendane na maadili ya kitanzania ya kuishi kwa unyenyekevu, upendo,
ushirikiano na kuheshimu watu.
Wito
huo umetolewa hivi karibuni na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati
wa futari ya pamoja iliyoandaliwa na chama cha watanzania waishio nchini
Botswana (ATB) katika hoteli ya Grand Palm mjini Gaborone nchini humo.