RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AZURU WILAYA YA SEGEREMA
Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akivishwa skafu kutoka kwa chipukizi mara tu baada ya kuingia wilayani Sengerema kwa ziara ya siku moja tarehe 10.9.2013.Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Katunguru kilichoko wilayani Sengerema alipokwenda kijijini hapo kwa kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa Katunguru/ Nyamtelela tarehe 10.9.2013.Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa Katungulu/Nyamtelela utakaogharimu shs milioni 734 na utawanufaisha zaidi ya watu elfu kumi.Rais Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Luchili akiwa njiani kwenda katika kijiji cha Bukokwa kuzindua rasmi mradi wa umeme tarehe 10.9.2013.Wageni waalikwa wakifuatilia kwa makini sherehe za uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini uliofanywa na Rais Kikwete huko Bukokwa wilayani Sengerema tarehe 10.9.2013.Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokea hati ya makabidhiano ya mradi wa umeme wa Bukokwa uliofadhiliwa na Millenium Challenge Co-operation ya Marekani.Rais Jakaya Kikwete akiangalia michoro inayoonyesha usambazaji wa umeme katika mkoa wa Mwanza.Rais Dkt. Jakaya Kikwete akizindua rasmi mradi wa umeme wa Bukokwa tarehe 10.9.2013
PICHA NA JOHN LUKUWI
No comments:
Post a Comment