Tuesday, September 17, 2013

KUFUATIA ZIARA YA KINANA SHINYANGA CHADEMA WAWEWESEKA!

na1Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza na waandishi wa habari katika kijiji cha Mwandoya leo Wilayani Meatu ambapo alifafanua mambo mbalimbali kuhus Shutuma zilizotolena Chadema kuhusu Balozi wa China nchinina2Waandishi wa habari wakimsikiliza Nape Nnayue wakati alipokuwa akizungumza nao katika kijiji cha Mwandoya.
………
~. Kinana: tuna deni la kuwatumikia wananchi sio kulumbana.
Kasi ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha 2010/2015 yaibua makubwa kwa vyama vya  upinzani hasa Chadema. makubwa hayo yamedhihirishwa na   shutuma za Chama hicho kwa balozi wa China nchini kwa uamuzi wa nchi hiyo kuwekeza kwenye viwanda vya pamba na mazao yatokanayo na mifugo kwa mkoa wa Shinyanga.
Katika mkutano wa Chadema na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Chadema walidai kitendo cha Balozi wa China Dk. Lu Youqing kushiriki katika mkutano wa hadhara wa CCM mjini Shinyanga ni cha utovu wa nidhamu, uvunjifu wa sheria hoja ambazo hazina mashiko.
Hata hivyo Katibu wa NEC ya CCM itikadi na uenezi Ndg. Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari kijijini Mwandoya, wilayani Meatu mkoa wa Simiyu kwenye ziara ya Katibu mkuu wa CCM mkoani humo aliwataka watanzania na wanakanda ya ziwa kuzipuuza shutuma hizo dhidi ya balozi wa China na akawataka waendelee kuunga mkono juhudi za CCM za kutekeleza ilani yake ya uchaguzi.
“tatizo la hawa Chadema wamezoea kufanya harakati zao kwa kutumia matatizo ya watu, sasa leo juhudi za CCM kutatua tatizo la bei ya pamba na soko lake inawanyang’anya mtaji wao muhimu sana ndo maana wanapiga kelele. Lakini pia tatizo la ajira kwa vijana wao walikua wanalitumia kama mtaji wa kupata waandamanaji, sasa vijana wakipata ajira kwenye viwanda hivi ambavyo vitaanza kazi Desemba mwaka huu, watakosa waandamanaji ndio chanzo cha kelele zote hizi” alisisitiza Nape
Nape alisisitiza kuwa vyama vyote vya siasa vina vyama rafiki kutoka nchi mbalimbali duniani, lakin tofauti inakuja kwenye aina ya urafiki husika, na kutoa mfano wa tofauti ya urafiki kati ya Chama Cha Kikomunisti cha China na CCM kuwa umelenga katika shughuli za maendeleo, lakini kwa upande wa Chadema ni tofauti.
Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Kinana amekuwa akisisitiza mara kadhaa kuwa CCM ina deni kubwa la kuwatumikia wananchi katika kutimiza ahadi zao kwa wananchi walizozitoa kupitia ilani ya uchaguzi ambayo watanzania waliichagua mwaka 2010 na ahadi mbalimbali za wagombea wa CCM.
“sisi CCM tuna kazi ya kuwatumikia wananchi,kutimiza ahadi zetu kwao na sio kulumbana na wapinzani. Na hii ndio tofauti ya chama kilicho madarakani na vyama vya upinzani, wakati wao kila kukicha wanatafakari wazungumze nini sisi tunahangaika kuwatumikia wananchi waliotupa dhamana ya kuongoza nchi yetu.

No comments:

Post a Comment